24 June 2010

MALARIA


MUHESHIMIWA NA MUOGOPWA MR MBU AKA MOSQUITO

MALARIA:Ni ugonjwa unaosumbua sana katika nchi za ukanda wa joto au (tropical countries),ugonjwa huu umeshaua na bado unaua watu na hasa watoto.Kinga halisi bado haijapatikana bali huwezwa kukingwa kwa muda mfupi na pia kutibika.Mbu ndiye mdudu anayesumbua sana katika maambukizi kwa kuwadunga watu, huyu jamaaa ni noma sana na huwa hakosei akipata nafasi hufanya kweli.Wa England wana sema "one mistake one goal".Sasa basi katika nchi yetu ya Tanzania kuna miradi mingi imeanzishwa ili kukabiriana na hawa mbu na mmoja wapo kubwa ni kutoa msaada wa vyandarua(mosquito nets)kwa wananchi ningependa kulipa swala hili kipau mbele kwa nia ya kuweza kupata nafasi ya kuwajumuisha wanajamii ya kitanzania waishio nje za nchi na hasa UK kuweza kunipa taarifa yoyote jinsi ya kufanikisha uhamasishaji wa utoaji msaada ili vyandarua viwe rahisi na kuwafikia walengwa katika muda muafaka...kama una maoni basi wasiliana na HUNGAZ ili tuonyeshe upendo ..nimefurahishwa sana na hamasa ya wasanii hawa katika video hii ambayo ukiangalia na kuisikiliza vyema utaguswa sana karibu na tuwe pamoja sana wana wane.

No comments: