23 July 2010

TOKA TANZANIA HADI UK

 
Ndugu wana blog leo nilipata nafasi ya kuongea na watu mbalimbali waishio hapa United Kingdom.Katika maongezi ya kawaida tu niliweza kuuliza maswali machache yanayo husu maisha yetu watanzania tuishio huku na Uraia wa nchi mbili utasaida waghaibuni kwa jinsi gani.Kila mtu alitoa majibu na maoni yake,Nilijaribu kuyachambua majibu na maoni hayo na kuafikia mtazamo wangu kama ifuatavyo;
Tulio wengi tulikuja kwa njia halali japo katika njia hizo nyingi zilihusisha mbinu mbalimbali za kiusanii kama unavyojua"bhatoto bha mujini".Kwa wanao kumbuka jinsi ilivyokuwa vigumu kusafiri kuja nchi za nje wakati wa uongozi wa mzee mchonga miaka ya toka uhuru hadi 80's.Ilikuwa ni lazima uwe una kuja masomoni na sponsor ilikuwa ni serikali,au uje kwa ajili ya matibabu au kwa shughuli za kidini na kikazi.Kipindi cha badiliko kilipotokea pale Uongozi wa Rais wetu mstaafu A.H.Mwinyi kuingia madarakani,na migogoro ya mfumo wa vyama vingi kilisababisha watu wa kila kiwango kutiririka kama maji ya mto yaingiapo baharini.Sasa basi baada ya kufika huku na kukuta mambo tofauti na fikra na matarajio yetu? maisha yetu yamukuaje? na tumeathirika au fufanikiwa kwa kiasi gani?? Habari zaidi zinakuja ila kwa sasa unaweza kuchangia ili nitakapo wakilisha habari nzima kila msomaji atakuwa ameridhika na mtazamo wa hungaz.so uliza swali au toa maoni yako hapo chini. asanteni

PIA TUPIA MTAZAMO WAKO JUU YA URAIA WA NCHI MBILI NA JE PASSPORTS HIZI ZINA MSUKUMO GANI WA MAENDELEO YA WAGHAIBUNI??
Angalia Mh Balozi Membe na balozi wa Tanzania Uk akilizungumzia swala hili






Ukiziangalia pass hizi kwa haraka haraka utazitofaulisha kwa rangi,kati ya nyekundu(UK) na kijani (TANZANIA).Kiundani tofauti ni kubwa mno hasa kwa wakazi wa hapa wenye asili ya kwetu TZ.Kwa mtazano wangu wa haraka haraka naona tofati na faida zake ni katika "USALAMA WA RAIA na"UCHUMI WA RAIA" i.e "citizen's security" and "citizen's finacial surport".Ila huu ni mtazamo wangu tu ki muhtasari mengi yapo kwenu kwa hiyo tuelimishane bila aibu kwa kuongea ukweli kwani muda wa kupretend haupo tena sasa, Ni bora kuelimishana mapema maana bado kuna watu wanafikra ambazo bila kusaidiwa wana weza kutumbukia kwenye dimbwi la msemo wa "BORA KUZALIWA PAKA ULAYA KULIKO BINADAMU AFRICA(TZ)na kusahau kabisa msemo mwingine wa "MKATAA KWAO NI MTUMWA"....changia .Nadhani wote mnao safiri kwa maborder ya nchi mbalimbali za ulimengu, mnaweza kukubaliana nami juu ya uchambuzi na utengwanishaji wa Raia wa nchi tofauti unavyokuwa kama "chuya zinavyo pembuliwa kutoka mwenye mchele"na hasa ukiingia kwenye UK borders. !!!!!!!!!!!

No comments: