Marehemu Syllersaid Mziray |
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU MZIRAY
Mziray alianza kazi serikalini 1981 akiwa kama Afisa Lugha na Sanaa wa Wizara ya Utamaduni na Michezo kabla ya upandishwa cheo na kuwa Mtaalamu wa Soka Wizarani 1986.
Alichukuliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani kama mhadhiri wa kitivo cha Elimu ya Viungo (Physical Education) lakini baadaye akaajiriwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania akiwa ni mmoja wa wahadhiri wa masuala ya kijamii.
Itakumbukwa alikuwa na ndoto za kuanzisha Chuo cha Soka, ili kuinua mchezo huo hapa nchini na mara zote alikuwa akilia na program za vijana.
Mziray alizawaliwa Novemba 11 mwaka 1957 na kupata elimu ya msingi katika shule za Ifunda (Iringa), Lpw Academic (Iringa) Mpechi (Njombe), Songwe (Mbeya) Butimba (Mwanza) Lukajunge Karagwe) na kumalizia Wami (Morogoro) mwaka 1973.
Alisoma Sekondari ya Malangali na kidato cha tano na sita alisoma Sekondari ya Mirambo mkoani Tabora na baada ya kuhitimu, alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Makutupora mkoani Dodoma iliyokuwa kwa mujibu wa sheria.
Mwaka 1981, alikwenda kozi mbalimbali nchini Bulgaria na kuhitimu 1986 na alipata shahada ya pili ya viungo na utamaduni.
Alikwenda Norway mwaka 1996 na 1997 kwa kozi nyingine na 2000 alikwenda Finland akiwa mwanafunzi wa Chuo cha Vuebamaki.
HUNGAZ TUNATOA POLE KWA NDUGU NA WAPENZI WOTE WA MICHEZO R.I.P SUPER CAOCH WETU
No comments:
Post a Comment