30 November 2010

HIVI TUTA AU MATUTA YA KUPUNGUZA SPEED YANAGHARIMU KIASI GANI?

Hii inasikitisha sana!! Wahungaz naomba leo tuliangalie swala la usalama wa raia kwenye barabara zetu pale home TZ.Hivi kweli serikali inashindwa kufuatilia swala hili hadi mpaka wanafunzi wanaamua kuandamana? inasikitisha.Katika tukio la hivi karibuni ambapo mwanafunzi wa Azania  aligongwa na gari  mitaa ya Barabara ipitayo mbele ya shule za sekondari za jangwani na Azania kuelekea Muhimbili.Jambo hili linakera na kuonyesha jinsi muundo wa utendaji kazi kuanzia ngazi ya wilaya hauna msisitizo na muamko.Ukiangalia taarifa ktk video ya hapo chini utapata picha kamili juu ya swala hili la kusikitisha,Na zaidi ni pale wanafunzi hao walipoanza kukamatwa na jeshi la police...angalia jinsi wanavyo pigwa mambata utadhani wezi bwana....noma. sijui ndugu wahekimika mna hekima gani kwenye kutoa ushauri wa jambo hili ambalo utatuzi wake haugharimu mamilioni bali moyo wa utendaji kazi muafaka.

No comments: