10 December 2010

DIAMOND APASUA JIPU BBC

URBAN PULSE CREATIVE Ikishirikiana na BBC inapenda kuwaletea Mahojiano kati ya Msanii Wa Kizazi Kipya Diamond na Mtagazaji Fred Mtoi kutoka BBC yaliyofanyika ndani ya Studio za URBAN PULSE NA BBC hivi karibuni na kuruhwa duniani kote. Diamond alipata fursa ya kuwashukuru kwanza URBAN PULSE kwa kumfanikisha kufika UK kwa mara ya kwanza, watanzania wote pamoja na wafans wake mbalimbali waliojitokeza kuja kwenye URBAN TOUR to support war against Malaria. Licha ya hapo pia aliweza kutoboa ukweli wa jinsi gani wasanii wa kibongo wanavyonyaswa na taasisi mbalimbali pamoja na wasambazaji ambayo huwatumia na kuwanyima haki zao za malipo wanayo stahili.



Aidha Diamond aliongeza kwa kuiomba Serikali Ya Tanzania Kuingilia kati swala hili Sugu kwa kuijali na kuisaidia Tasnia ya musiki wa bongo fleva na Filamu ili kuwaendeleza wasanii na kuingizia serikali kipato kikubwa badala ya kuwaachia maharimia sugu kuendelea kuwaibia kazi zao wazi wazi.



Video hii imetengenezwa na URBAN PULSE.
Asanteni
URBAN PULSE CREATIVE

No comments: