3 December 2010

MZUNGU ALIYEFUZU MAFUNZO YA UNYAGO PALE ZANZIBAR HUYU HAPA

Midundo ya asili ya muziki wetu ,inavutia sana watu wengi nje na ndani ya TZ , na wengi huenda Tanzania au Sehemu mbalimbali kwenye vyuo kama Bagamoyo ili kujifunza utamaduni wetu.Sasa wadau nimeamua kuiwega video hii makusudi ili wasiofahamu kwamba mguso wa mirindimo ya nyimbo na styles za uchezaji hugusa wengi bila kujali mipaka ya Rangi au jinsia.Tukiangalia ndani sana ya mitindo ya unenguaji kama chakacha,Vanga,Taarabu aka mduara mnaweza kukubaliana nami kwamba Dada huyu hapo chini amehitimu elimu hiyo.Kwa mtazamo wangu naamini ART haina mpaka Iwe uchoraji,Uandishi,Usimulizi, muziki n.k vyote hivyi hulenga na kufundisha jamii kwenye anga zote iwe kwenye negative au positive ideas.Nijukumu la mtu mwenyewe kuchagua kipi chema  kwake, kwani upeo wa fikra huhitimishwa na maamuzi ya mfikiriaji.Ni hayo tu



Video hii hapa chini inathibitisha mtazamo wangu.Ni nyimbo aliyo katika maadhi ya mwambao ambayo ameimbwa kwa mafumbo ya lugha tamu ya kiswahili,sasa wana hunga naomba mjionee wenyewe jinsi wakina dada wanavyo kata mauno.Je kuna tofauti na dada wa kizungu aliepagawa na style hii mahiri?Nadhani tofauti ipo kwenye mavazi tu na hii nikutokana na asili ya wahusika,mavazi ya wenzetu yana eleweka,vilevile kwa mwambao ila ujumbe wa ukatikaji uko palepale
Nyimbo hii inaitwa BATA  imeimbwa na Mzee Yusufu kushirikiana na Offside Trick .

No comments: