Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Steven Kanumba(The greatest) ameamua kufanya kweli mwaka huu.Msanii huyo ambaye kwa sasa yuko mapumzikoni nchini Marekani amefafanua kwamba anajiandaa na makamuzi ya kufa mtu mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata kupitia libeneke lake zina kamilisha habari hii kwa kuonyesha picha za shooping ya baadhi ya vifaa vipya kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kampuni yake ya utengenezaji wa filamu iliyopo pale TZ.
|
Kanumba akiwa ndani ya duka la B&H New york |
|
Duka la B&H kwa nje |
|
Cameras katika moja ya kitengo cha duka hilo |
|
Kanumba akitoka na baadhi ya vitu alivyo nunua |
|
Mbali na The Greatest kuwa likizo USA kazi zinaendelea kama kawaida ofisini kwake na mwezi huu kwa kuanza mwaka anaanza na movie iitwayo...''DECEPTION, movie hii ina tarajiwa kuwa mtaani soon...Kanumba ameongeza kwa kusema hivi". Kwa mashabiki wa kweli na wazalendo inatakiwa kununua copy original na si feki,lakini pia hawaazimani bali kila mtu hununua ya kwake tena original.''Mkataa kwao ni mtumwa''..''Mcheza kwao hutunzwa'' ''Tusitukuze vya nje na kudharau vyetu maana upendo wa dhati huanzia nyumbani na si ugenini,tujikubali sisi wenyewe kwa kupeana mioyo na kushauriana kwa njia na nia njema bila kutukanana wala kupondana maana lengo letu ni zuri kwa jamii aliongeza msanii huyo
PATA NAKALA YAKO MAPEMA
kwa habari zaidi unaweza kumtembelea kwenye link hizi; http://kanumbathegreat.blogspot.com/ na pia katika wesite yake hapa; www.kanumba.com |
No comments:
Post a Comment