Pacha Izz kushoto na kulia ni Pacha Jaco B Habari zilizotufikia Kupitia website inayoogoza ktk anga za burudani pale Tanzania www.bongostarlink.com chini ya DJCHOKA,zinasema kuwa msanii kutoka Watengwa Pacha Izz amefariki dunia usiku wa kuamkia leo maeneo ya Clock Tower-ARUSHA kwa kupigwa kisu. Inasemekana Izz alikuwa anatokea club Mawingu wakati anarudi home akakutana na machangu doa, marehemu Izz aliongea nao na kuwaambia kwanini mnatukanatukana ovyo ndipo changu mmoja alipomchoma kisu ubavuni na kufariki hapo hapo. Dada huyo alikamatwa na kupelekwa kituo cha police lakini baada ya mama mzazi wa Izz alipoambia aliomba dada yule aachiwe huru. Pichani kuanzia kushoto wapili ni DJ CHOKA na kushoto(aliyefunika kichwa) ni PACHA IZZ,kwa mujibu wa Choka, yeye ndie aliyeMpeleka hapo kwenye kaburi la father Nelly(x- plasterz member aliye uwawa kwa kisu pia) na kumzungusha Kijenge(Arusha) walikuwa marafiki sana na kila mara walikuwa wakiwasiliana kwenye simu kuhusiana na project yake ya mziki. ""Sasa ndoto zote zimezimwa aisee daaah nenda tu Izz katuandalie makazi kichaa wangu"" aliongeza Choka. HAPA WATENGWA WAKIKAMUA Hungaz nimeona msiba wa kachaa dah man Choka, pole sana...imenistua na kuniuzunisha sana...sijui kama sababu ni ya kweli maana nawajua wana wa AR...dah mambo ya visu huku UK ni kawaida kuliko Gun..inasikitisha Watanzania tunaingia kwenye level hii na naona inapanda kwa kasi...dah.Hakuna wakuhukumu zaidi ya mola kaka.pole CHOKA, na kwa familia nzima ya marehemu PACHA IZZ R.I.P |
11 March 2011
BURIANI PACHA IZZ WA WATENGWA-ARACHUGA TZ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment