21 March 2011

TATIZO LA UMEME TZ-Kinyesi cha binadamu kukomboa wananchi???

TATIZO LA UMEME TZ:

Wajameni hili swala la umeme pale home linaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kiasi fulani.Kuna mdau mmoja amenipa habari hiii, ""Kinachotakiwa ni watu kula sana. iliwaweze kwenda haja kubwa kwa wingi"".eti kama kuna umeme na gesi unaotolewa na wanyama(ng'ombe) basi hata binadamu wanaweza kufanya hilo.
Alisisitiza kusema kama serikali ikiruhusu watu wajitengenezee umeme wao basi hakutakuwa na haja ya kusumbuana katika mahitaji madogo madogo kama mwanga,gesi ya kupikia n.k.Sasa kwa wale wanaohitaji kwa ajili ya kuendesha mitambo yao jamaa aliongeza kwa kuwashauri wakodishe watu zaidi au wale zaidi ilikukidhi mahitaji yao.
KWA SERIKALI: Jamaa alisema kwamba watumie umeme unaozalishwa kwaajili ya viwanda bila kuwapa mgao na Wavitoze viwanda hivyo kodi kufidia kodi ambayo wananchi wachini wamekuwa wakiichangia kwa kulipia umeme wanaonunua.
Mdau aliendelea na kusema,"Pia serikari itoe mafunzo maalumu na kurahisisha upatikanaji wa vifaa husika kwa kusaidia vyanzo hivyo kutumika kirahisi na kwa bei poa.
MTAZAMO WANGU:
Mdau!!kweli umekerwa na dhahama hii ya mgao wa umeme.Kuwafanya watu wale sana na kwenda haja sana ili wachangie rasilimali kwa ajili ya uzalishaji wa njia hii ni kuwazalilisha watu. Na je! hicho chakula kitapatikana wapi wakati watu wanakufa na njaa??? na pia mfumo huu mzima unahitaji maji ya kutosha na hali ya ukame ni tatizo pia.Dah mimi naona ni bora utafute wazo lililo la maana zaidi kuliko hili japo kuna kapointi kidogo ndani yake.
MTAZAMO WAKO:
Wajameni habari ndio hiyo sasa wewe kama muona mbali!!? Swala hili unalionaje?na je una lakumshauri ili mdau aweze kufarijika na kuachana na taaluma hii na kuweza kufuatilia ufumbuzii mwingine????
toa maoni yako!!!!!-HUNGAZ (www.hungaz.blogspot.com)

No comments: