27 April 2011

SIKU YA MUUNGANO NA MTAZAMO WA RAIA WA TANZANIA

Rais Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dr. Shein katika maadhimisho ya sikukuu ya miaka 47 ya Muungano.

MAMIA ya watu jana waliupamba Uwanja wa Amani, Zanzibar katika sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Watu hao walionekana kuvutiwa zaidi na mgeni rasmi, Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad.Umati huo wa watu, wengi wao wakiwa katika sare tofauti tofauti, ulilipuka shangwe za kelele na vifijo wakati viongozi hao wawili walipoingia kwenye uwanja huo kwa nyakati tofauti.


Rais Kikwete aliingia uwanjani hapo majira ya saa nne asubuhi akiwa kwenye gari la wazi na kuwapungia mkono mamia ya wananchi na baadaye kukagua gwaride.Baada ya hapo gwaride lilipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa kasi na kisha mwendo wa pole.

MAONI NA BAADHI YA MICHANGANUO YA WADAU ;
  1. [Toka ZANZIBAR]; Watanganyika choyo roho mbaya zimekushikeni.ZAnzibar tukijitenga hatuto pigana maana uunguja upemba hizi ni fitina za watanganyika nyinyi kwenu muna makabila 200 kwa hiyo kesi za ngombe tu munapigana aridhi munapigana piya kuna uisilamu na ukristu sasa kazi kwenu na ujerumani ulaya yote huchukuwa gesi russia licha ya kuwa nato ni mpizani wa russia
  2. [Toka TANGANYIKA]; Tatizo lako ni fikra bubu.Na usicommite general fallacy (watanganyika) usifikiri kila mtanganyika anaipenda zanzibari. ili iweje?Nyie tenganeni mkaungane na libya, who cares? i care for my family not your kisiwa.
    wewe ni bunguwani!


    Haya wadau wangu hiyo ndiyo hali halisi ya fikra za baadhi ya watu juu ya muono wao kwenye muungano wa nchi yetu nzuri ya TANZANIA.Katika habari hii ambayo ningependa mchangie ni wazi kabisa kwamba kila mwananchi anahitaji kuona ufumbuzi wa swala hili kabla hatujapelekana mbali. Namalizia kwa kuwapa taswira ya mdau mwingine aliye changanua wazo hili kama ifuatavyo;
TOKA KWA BWANA KADIO:
Muungano maana yake nini?muungani maana yake ni makubaliano ya nchi fulani kuungana na nchi nyingine kiuchumi kisiasa na kiutamaduni...bila kujali itikadi ya mtu anakotoka.,,..kuungana ni kuwa kitu kimoja kukusanya nguvu ya pamoja na kusema haraambeee!!!au wanaumeee!!!the n kupush jabali lile lenye kukinga mianya ya maendeleo,..mtu anaye jua maana ya muungano hawezi kujitenga labda kama hajaenda shule kutoa ule ulimbukeni na kuweka dira ya utashi...tanganyika iliungana miaka michache tu..wakati ulaya waliungana zaidi ya miaka miambili iliyopita..kwasababu walijaa utashi wa kuona mbali..sasa wenzetu wametuacha wapi?....nchi makini huungana ili kuweka nguvu kiuchumi sanasana...,,..miaka ya nyuma SIR MARCUS GAVEY SAID..AFRICA MUST UNITE!..kinachotokea kama huja unite ni kwamba huwezi ku tread bila kupunjwa kwasaba wenye masoko ulaya hukupangia bei..lakini kama africa tuki unite then tutawaambia mnanunua kwa bei hii na watanunua kwani hawana pa kukimbila..lakini sasa wewe kama ni independent tu ..ukisema nunua kahawa yangu kwa bei hii then watesema kama hutaki tutenda nunua kenya...,lakini ukiwa unite then mnapanga bei na wata nunua tu..,usalama pia ni muhimi ndio maana tunaonewa na mataifa ya magharibi kwasaba tuko independent hatuna nguvu ya pamoja....si kupiga kelele kamahujui bora kunyamaza...msomi hawezi kusema tuvunje muungano bali atasema ufanyiwe marekebisho ili uwe imara ..kwasababu ukivunjwa hamtaupata tena pale mtakapogundua mamefanya makosa kufanya hivyo...maswala ya uzanzibari au utakanganyika futilia mbali kwani historia inasema wazanzibari ni walewele watanganika walio hama wengine kuchukuliwa kuwa watumwa kunyanyaswa kama wanyama na waarabu..na si kificho hiyo ndiyo kweli.....lakini kwa mstakabali huu hatuendi kwakufuata au kuishi tukitazama nyuma bali hujenga imani ya undugu ili kujenga nchi iliyo imarika...kuishi bila chuki au kubaguana kwa rangi au unakotoka ndiyo misingi imara yenye tija katika kujikomboa na umasikini uliokidhiri,kuf anya kazi kwa bidii na kupanua mitaala ya maendeleo bila kujali itikadi zenye mgando wa akili.,zanzibar and Tananyika must progress to make the unite strong,desroy all the evils against humanity, building up one nation of eaqual ,rigths and justice.
Chanzo: www.mwananchi.co.tz

No comments: