15 May 2011

Polisi wahaha kumnasa muuaji wa wanawake

WAKATI watalaamu wa Saikolojia wanasema mtu anayetuhumiwa kuua wanawake katika nyumba za kulala wageni jijini Dar es Salaam anakabiliwa na matatizo ya kisakolojia, polisi wamesema hawatalala mpaka wanamtia mbaroni.
Muuaji huyo ambaye mpaka sasa ameua wanawake zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, anaua kwa staili moja ya kuvunja shingo baada ya kutembea nao na kisha kuwaacha uchi.Kwa nyakati tofauti wakuu wa polisi wa mikoa ya Ilala, Temeke na Kinondoni wamezungumzia suala hilo na kusema kuwa wana mkakati maalumu wa kumnasa mtu huyo.
Hata hivyo, Mtalaamu wa Saikolojia ya Jamii ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa mlolongo wa mauaji hayo ya wanawake unaonyesha kuwa muuaji anakabiliwa na matatizo ya akili...........endelea hapa

Alisema kuna watu wachache katika jamii ambao wana matatizo ya kisaikolojia wakifanya mapenzi furaha inapowazidi huamua kufanya chochote ambacho kinaweza kumdhuru mwenzake.Dk Kitila alisema furaha ya watu wenye matatizo hayo ni kuona mwenzake akiumia na kwamba tatizo hilo likiendelea zaidi hufikia hatua ya kuua kila anapofanya mapenzi..............endelea hapa http://mwananchi.co.tz/mwananchi-jumapili/40-habari-mwananchi-jumapili/11912-polisi-wahaha-kumnasa-muuaji-wa-wanawake

No comments: