27 October 2011

Jestina akiwa katika pose na Tuzo yake
SALAM,
Napenda kutoa shukurani zangu za pekee kwa Mwenyezi Mungu, Familia yangu, Marafiki zangu, mashabiki wangu, wadau na watanzania wote kwa ujumla walioweza kunipigia kura ambazo zimefanikisha blog ya MissJestinaGeorge kuibuka kidedea na kunyakua ushindi mkubwa wa kuwa ''BLOG BORA YA MWAKA 2011''  katika tuzo za BEFFTA zilizofanyika nchini UK mapema wiki iliyopita.

 Mchakato mzima wa kumtafuta mshindi ulikuwa na changamoto lukuki ukizingatia ya kwamba kulikuwa na jumla ya blogs 15 za kimataifa kutoka nchi mbali mbali Duniani. Kutokana  na ushirikiano wenu mzuri  mmeiwezesha blogu yetu kupata ushindi mnono na vile vile kunipatia fursa nzuri ya kuiwakilisha vyema Tanzania Ughaibuni.
Ni vigumu kumshukuru kila mtu mmoja mmoja kwa mchango wenu uliosadia kuwezesha blog yetu kunyakua ushindi mkubwa ingawa ningependa kuwatambua wafuatao: kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu zote za dhati kwa  timu ya URBAN PULSE CREATIVE  kwa mchango wao mkubwa waliotoa, wanachama wenzangu wa AMTTA (Amka Mwanamke Twende Tujikomboe Afrika) kwa kuwa na mimi bega kwa bega nawapenda sana. Pia natoa shukrani kwa Bloggers wenzangu wote, tovuti mbalimbali, TONE RADIO popote pale walipo kwa michango yenu.
Nawasihi sana tuendelee kushikamana, kupendana na Kusaidiana kwa hali na mali ili isiwe tu kuleta maendeleo nchini kwetu bali pia kupeperusha bendera ya nchi yetu Tanzania Duniani kote.
Napenda kuitoa wakfu tuzo hii kwa dada yangu mpendwa Kissa George aliyetutoka
''I miss you so much Sis'' najua kama angekuwa hai angefurahia sana.
 Mwisho namshukuru sana binti yangu Iman ambae amekuwa nguzo na muhumili mkubwa katika maisha yangu kwa kunipatia nguvu za kuendelea mbele siku hadi siku.
Binadamu kushukuru ni wito ila leo umekuwa ni wajibu wangu.
 Asanteni sana,

Mungu awabariki sana na ninawapenda sana
Jestina George

No comments: