29 March 2012

JE WALIFAHAMU HILI;


Almasi zimekuwa mtama kwa wakina dada na hasa kwenye maswala aya mapenzi.Kwa watu wengi huamini kuwa Almasi ni alama ya utajiri yaani kwa kuvaa au ukimiliki almasi yenye uzito wa juu basi wewe Unazo. Leo nawapa kahabari kadogo tu ili upate kuelewa swala la “DIAMOND” au almasi na mazingira yake kwenye anga za biashara duniani.Vita baina ya wapendanao imetawaliwa na kito hiki kwa kutumiwa kama ishara au token ya hisia zao kimapenzi kwa wenza.iwe engagement(uchumba) au ndoa Kwa mujibu wa takwimu za gazeti la THE TIMES la Uingereza,Africa inaongoza kwa uzalishaji wa almasi kwa kutoa kiasi cha $8.5 bilioni wakati jumla ya uzalishaji dunia nzima kwa mwaka unakaribia $13 bilioni.
Angalia uchambuzi wa thamani ya almasi zilizo na bei ya juu duniani hapo chini:
  1. Mpaka sasa Almasi yenye thamani kulikozote hapa duniani inapatikana UK na imepewa jina la Khl-I-Noor Diamond,kutokana na ukubwa wake imekuwa vigumu kuipa bei yaani ni Priceless.
  2. Cullian I: inakadiriwa kuwa na thamani ya £200 million paundi(3,106.75 carants)ambayo ili gondolier na Thomas Evan Powell -south africa
  3. The Millennium Star £130 The Hope Diamond inakadiriwa kuwa kiasi cha £125-160 milioni paundi
  4. Mwaka 2010 Kampuni ya Laurence Graff ilinunua almasi ya thamani ya £28 milioni Kwenye soko la vidani au jewellery markets mahitaji bado ni makubwa yakiongozwa na makampuni ya Kimarekani kwa kiasi cha dola $25.1 Bilioni ikifuatiwa na china $7.b bilioni,huku Migodi ya Argyle Australia ikiongoza kwa ukubwa duniani kwa kuzalisha karanti 20milioni kwa mwaka. Source The Times-Uk

No comments: