28 October 2012

MABADILIKO YA KIUCHUMI YAONGEZA MAUMIVU KWA WAGENI UK(sehemu ya pili)

MAISHA YA UGHAIBUNI

Miaka mingi imepita toka niingie nchi ya mwingereza ambaye alikuwa mtawala wa mwisho wa Nchi yetu zama za ukoloni.Maisha ya hapa ughaibuni ni ya mnyang’anyano na hayana tofauti sana na nchi zingine hapa duniani.Kama mgeni nilifika nakuanza kujifunza jinsi ya kuishi kwa kufuata mfumo wa nchi hii.Ilikuwa ni ngumu kiasi maana kibali nilichopewa hakikuniruhusu kufanya mengi kwani kilikuwa ni cha Uwanafunzi tu. Mwanafunzi haruhusiwi kufanya kazi zaidi ya masaa 20 na kwa hali hii ikawa ngumu kukidhi mahitaji ya muhimu kama chakula malazi,mavazi na hata pango.Ni mpambano mkali si mchezo.

Nilitafuta kazi na kupata za vibarua tuu maana sikuwa na elimu wala uzoefu wa kutosha kuajiliwa kama mfanyakazi wa kudumu,mbali na hayo Uwanafunzi na uraia wa nje katu havikuwashawishi waajiri kutoa ajira.Sasa basi, kilichofuata ni mpango wa kuongeza kipato ili kukabiliana na hali Ya maisha ya hapa.Baadhi ya wenzangu waliweza kumudu kwani walikuja kwa njia ya serikali na wengine walilipiwa na wazazi wao ambao walikuwa na nyazifa kubwa na pesa nyingi nyumbani Tanzania .Mpango wa kwanza ulikuwa nikutafuta kazi mbili na kufanya masaa 20 kila moja ili kupata masaa 40 kwa wiki ambayo yangelingana sawa na kipato cha mfanya kazi wa kudumu wa kiwango cha chini. Hali hii ilihatarisha sana kibali cha kuishi nchini maana kama ukigundulika na vyombo vya dola kwa kuvunja sheria ya masaa 20 basi safari ya kurudishwa nchini kwako inakuwa imeiva.Sasa utata uja pale unapotaka kujisomesha ...elimu sio bure inahitaji ada na muda ,kama unafanyakazi muda wa masaa 40 kwa week ilikukidhi mahitaji ya msingi unapatawapi muda wa kusoma full time????.......Fuatilia habari hiii hapo baadae..kwa wale wenye maoni ya kumsaidia mdau huyu basi nitumie email hapa hungazblog@gmail.com ilitumsaidie mdau huyu.

No comments: