15 January 2013

MAMA KIKWETE NA SHERRY PARTY 2013




Mama Kikwete wa sita toka  kulia akiwa na wake wa mabalozi katika sherehe ya Sherry  Party 2013 iliyofanyika leo jioni pale ikulu Dar es alaam-(Picha toka Michuzi)
 Tafrija iliyotambuliwa kama SHERRY PARTY 2013 iliyo fanyika jana Pale Tanzania na kuhudhuriwa na wake wa viongozi wa serikali chini ya Mke wa raisi wa nchi hiyo Mama Salma Kikwete imefuatiwa na shukrani na msisitizo toka kwa first lady huyo kama usomapo hapo chini. Swala la afya bora kwa kizazi kipya ni muhimu kwa maendeleo ya baadaye ya taifa la Tanzania na sote twalifahau hilo..Mama amemalizia kwa kutoa ujume huu hapa ambao naunukuhu toka katika mtandao wa Facebook :  

 Alisema:



Salma Kikwete akiwa na baadhi ya wananchi
katika moja ya kampeni zake za afya kwa jamii
"Nawashukuru Mabalozi na Wenza wao kwa namna ambavyo wanaendelea kuwa na Imani na Serikali yetu na nchi yetu. Nawashukuru pia kwa namna ambavyo wamekuwa na mchango wa kipekee katika kuendeleza Taasisi yetu ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) na kuiwezesha kutimiza ndoto za watoto na Wanawake wa Kitanzania katika kukabiliana na changamoto za maisha ya kila siku.
NAWATAKIA HERI NA FANAKA YA MWAKA MPYA WA 2013,UWE MWAKA WA MUENDELEZO WA MAHUSIANO MAZURI KATI YA NCHI YETU NA NCHI MARAFIKI KATIKA MAENDELEO.

HAPPY SHERRY PARTY 2013."
Mama Salma akiwa na Mumewe
 Mh Rais Jakaya Kikwete
Kisha Mama aliendeleza msisistizo wake kwa kukandamizia na Ujumbe huu pia
" Mwanadamu yeyote hufarijika pale wenzake wanapompongeza kwa jambo lolote analolifanya,hususan lenye manufaa kwa jamii inayomzunguka. Leo nimepata faraja kubwa sana moyoni mwangu kwa namna ambavyo wenzetu wanaowakilisha nchi zao hapa kwetu Tanzania walivyoonesha kutambua Mchango mkubwa wa Taasisi ninayoiongoza ya WAMA,nimepata faraja pia kwa namna wananchi wenzangu wanaothamini kazi hizi tunazozifanya wanavyotoa maoni yao kwa njia mbalimbali ikiwemo hii ya Facebook.
WAMA ITANENDELEA KUWEPO KWA MANUFAA YA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI ITIKADI ZAO ZA KISIASA,DINI,RANGI WALA KABILA."

MTOTO WA MWENZIO NI MWANAO,MKINGE NA UKIMWI.


No comments: