8 March 2013

SIKU NI YA WANAWAKE DUNIANI TUITAFAKARI PAMOJA

Habari toka Tanzania Nchi Yetu Sote (M4C)
Hii ndio hali hali ya mwanamke mwenye kujituma.Kuna kila sababu ya kuwaunga mkono wanawake ili waondokane na maisha ya namna hii hasa katika nchi tajiri kwa rasilimali lakini maskini kwa viongozi wenye uzalendo 
Hongera kwa wanawake kwa kuiona siku yao Mungu awajalie muishi maisha marefu na kuzidi kufanikiwa mkiongezeka kimo na maarifa ya kuitambua haki yenu kuwa ni pamoja na kuandaliwa mazingira mazuri ya kupata elimu,huduma bora za afya,na haki ya kuzalisha na kumiliki mali. Pia Mungu awajalie mtambue kuwa nyinyi ni wengi na wingi wenu una madhara hasi na chanya hasa linapokuja suala la kufanya maamuzi yanayoamua mustakabali wa taifa zima kama vile kupiga kura. Inasemekana wengi wenu ndio hufanya chama tawala kiendelee kujivunia utafunaji wa rasilimali za umma bila hofu kwani wanajua mtaji wao ni mkubwa toka kwa kundi kubwa la watu wenye huruma ya asili hata kwa mambo yenye madhara kwa kundi husika.


Rai yangu ni kuwa mnayo haki na wajibu wa kupata haki lakini haki hiyo inapatikana tu katika nchi yenye viongozi wenye uzalendo na msingi mkubwa wa ukombozi wa mwanamke ni elimu kitu ambacho serikali yetu imekiri kwa maneno kuwa haiwezekani sio tu kupata elimu bure bali pia hata yenye ubora na uthibitisho unajionesha pale walimu walipojaribu kuomba watazamwe na wao kidogo kwani maisha ni magumu mno walitishiwa kufukuzwa kazi na wengine wakaambiwa wanaoona fani wanayoifanyia kazi hailipi wakatafute ajira kwingine na ndio maana wakaamua kuacha kazi na kubaki na ajira.

Wakati mnatafakari kuhusu siku yenu msisahau kujiuliza juu ya twiga na meno ya tembo nyara za serikali je zinamnufaisha nani? Je kuna sababu yoyote inayoweza kueleweka hata kufanya watanzania wanaozunguka migodi ya madini kuwa maskini wa kutupwa?

Aidha nawaomba mtumie siku yenu kutafakari jinsi ya kujiletea maendeleo nyinyi binafsi na taifa kwa ujumla badala ya kujazana kiburi na jeuri ambavyo mwisho wake ni kuvunjika kwa ndoa nyingi na mifarakano isiyo na tija.

No comments: