17 July 2013

ABUSE: Je ni mila na desturi zetu? au ni ujinga wa kutojua maana ya kupendana.? Je wazazi huchangia maumivu ya maisha ya watoto wao? toa maoni yako.

Kuna wazazi wengine wanadhalilisha sana familia zao na kuziweka katika mazingira magumu ya dhihaki,matusi na aibu toka kwa jamii na kuna wakati inafikia mpaka mtoto kusema anatamani asingekua na mzazi kama huyo kwani mzazi mmoja anaweza akawa anamdhalilisha sana mzazi mwengine na watoto wake kijumla na mwisho wa siku watoto wengi hujenga imani ya kuwachukia sana wazazi wao na kuwadharau sana wazazi wa dizaini hiyo,,hii inatokana na mzazi kukosa heshima na adabu kwa ndugu zake,jamii husika,familia yake kijumla..mzazi kutukana matusi ya nguoni mbele ya hadhara na kuwadhalilisha kwa matusi makali ya nguoni mke na watoto halafu mwisho wa siku anatembea kifua mbele huku akililia heshima kwa watu hao..mzazi kama huyo huishiwa kutukanwa na hata watoto wake matusi makali ya nguoni cz alikua anawatukana hao hao watoto wake matusi makali bila kujua nao ni human beings na wanaumia sana..inasikitisha na naongea hv nikiwa na ushuhuda wala sijaropoka.
.
This documentary is based on the response to situation of abuse and violence that children face. The response is in line with the launch of the report on Violence Against Children (VAC). The VAC report is Tanzania's responce to the United Nation's Secretary General's call for action to end Violence Against Children. Tanzania became the first country to respond to the call through undertaking a population based survey on situation of violence against children.

This documentary shows the reality of the violence that children go through and the effort taken by the Ministry of Community Development, Gender and Children and the Ministry of Health and Social Welfare with all the partners in helping eliminate and educate the community on Violence Against Children.


Makala hii inaonyesha ukatili dhidi ya watoto na jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na Wizara ya Afya an Ustawi wa Jamii wakishirikiana na wadau mbalimbali kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.Makala hii imetengenezwa ikiwa ni mwitikio wa hali ya unyanyasaji na ukatili ambayo watoto wanakabiliana nayo. Makala hii imeandaliwa sambamba na uzinduzi wa ripoti ya ukatili kwa watoto ambalo ni agizo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutokomeza ukatili kwa watoto. Ripoti hii ilizinduliwa na Dr. Asha Rose Migiro, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

No comments: