9 December 2013

Tanzania celebrates 52th Independence day today.

GREETINGS FROM LEADERS & FRIENDS

Hon Fredrick Sumaye.
Napenda kutoa salamu zangu za pongezi kwa Mh Rais Dr Jakaya Kikwete na watanzania wote kwa kutimiza miaka 52 ya uhuru wetu wa iliyokuwa Tanganyika na sasa Tanzania bara.
Watanzania tunamengi ya kujivunia kama Taifa katika miaka 52 ya uhuru wetu yapo mengi yaliyopatikana na yapo mengi yanayoendelea kutendeka katika kipindi hicho,muhimu sana katika kipindi hicho ni nchi yetu ni umoja, amani , utulivu na mshikamano kama Taifa. Tushirikiane na serikali yetu,taasisi zetu za kidini,kijamii,na wadau wote wa maendeleo ili kurahisisha maendeleo na utoaji wa huduma bora kwa jamii, pia tushirikiane na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuondoa maovu kama rushwa ,ufisadi,madawa ya kulevya,ujambazi ,mauaji na mambo mengine yanayoumiza jamii
Vijana ni nguzo ya rasilimali watu,tuwaamini ,tuwawezeshe na tuwatumie kwa manufaa ya Taifa letu

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

source; Fcbook

No comments: