- Kwa mujibu wa taarifa fupi tulizozipata hivi sasa za uchaguzi wa kata unaofanyika pale nyumbani TZ zinasemaa:
- Chama cha CHADEMA kimeshinda Kata ya Partimbo na Loolera za Kiteto mkoani Tanga,
- CCM YASHINDA UBAGWE: Hamisi Majogoro wa Kata ya Ubagwe wilayani Kahama ameshinda udiwani kwa kura 323, Adam Ngoma wa Chadema kura 219
- CCM imechukua Kata ya Kiomoni Mkoani Tanga
- CCM imeshinda kata ya Nduli Iringa mjini. Mh. MsigwaPeter aliwekwa ndani polisi kwa masaa matatu wakati uchaguzi unaendelea.
- Godbless Lema wa Chadema apigwa na kuumizwa vibaya na polisi Arusha
- CCM wamechukua Ludewa
- CHADEMA wameshinda Kiboroloni
- CHADEMA wameshinda Kiteto. Hii ilikuwa kata ya CCM
- Kutoka Ukumbi, Kilolo:
Vituo vyote vya kupigia kura vimeshafungwa. Shughuli ya kuhesbau kura inaendelea. Kamanda Nyalusi anasema hali iko shwari hadi muda huu. Polisi wamemuachia mgombea wa CHADEMA, mpiganaji Oscar Ndale, lakini wameendelea kuwashikilia makamanda kadhaa, akiwemo Kamanda Mwambigija (Mzee wa Upako) pamoja na gari la M4C.
Matumaini ya ushindi hapa ni makubwa. Baada ya gari kukamatwa. Vijana wa bodaboda wamejitolea kwenda kuziba nafasi hiyo na kujitoa kufanya kazi kuhakikisha mapambano ya kumpata kiongozi wao hayakwami.
Kurugenzi Ya Habari CHADEMA
9 February 2014
Matokeo ya uchaguzi wa kata Tannzania leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment