18 March 2014

Hivi ndivyo alivyo conclude kamanda Jesca Kishoa. wa CHADEMA




Unapotaka kujua uwezo na uimara wa mti, ni pale unapoona upepo mkali unavuma kwa nguvu lakini mti ule unasimama imara na kuruhusu upepo ule upite bila madhara.Chama changu kimepitia changamoto nyingi ambazo kwa upande wangu ninaamini changamoto hizo zinakiimarisha zaidi.Kuhusu uchaguzi wa Kalenga, natoa pongezi kwa makamanda wote wa chadema.Kazi iliyofanyika Kalenga ni kubwa na nzuri sana ya kujenga chama.Ikumbukwe mwaka 2010 chadema kalenga ilipata kura 900 na kitu, ila kwa sasa imepata kura 5000 na kitu.Hii ni hatua kubwa sana.Kubwa na la msingi ni vijana wote tuone umuhimu wa kujiandikisha kupiga kura.Mimi binafsi nilikuwa wakala, nimeshuhudia kati ya watu 115 waliopiga kura, vijana walikuwa 7 tu.Wengi walikuwa wazee wetu kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea.Na wengine hawakujua hata kupiga kura cha ajabu vitambulisho vyao vina signature na vilionekana vipyaaa..!!!Vijana wetu kama 70 walibaki nje wakisubili matokeo halafu washangilie.Kamwe huwezi kuvuna usichopanda.NACHUKUA FURSA HII KUWAHIMIZA VIJANA WENZANGU KUJIANDIKISHA ILI KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUFANYA MABADILIKO.BINAFSI BADO NNA IMANI KUBWA NA CHAMA CHANGU NA KUPITIA UCHAGUZI HUU IMETHIBITIKA KUWA CHADEMA NI CHAMA CHENYE NGUVU NA CHENYE UWEZO WA KUSHIKA DOLA.HAKUNA KURUDI NYUMA MBELE DAIMA...! PIPOOOOOZ..!

No comments: