1 December 2010

ZANZIBAR HEROES WAAHIDI KUIFUNGA IVORY COST LEO..GOOOD LUCK!!!


Nadir Haroub Cannavaro

USHINDI wa mabao 2-0 ilioupata Zanzibar Heroes dhidi ya Sudan, umempa jeuri nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub Cannavaro ambaye ametamba wataichapa Ivory Coast leo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Zanzibar inatarajia kuingia uwanjani leo kukipiga na wapinzani wao hao kwenye Uwanja wa Taifa, mechi itakayokuwa na upinzani kwani Ivory Coast wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao 2-1 na Rwanda katika mchezo wao uliopita.
Cannavaro, beki wa klabu ya Yanga aliliambia gazeti hili kuwa wanajivunia ubora wa kikosi walichokuwa nacho, na ana hakika watashinda mchezo huu na kufanikiwa kufuzu kwa hatua ya makundi .(habari na Na Wilbert Molandi)....Soma zaidi hapa

No comments: