2 February 2011

KIFO CHA MAMA HUYU NI AIBU KWA SERIKALI

Taarifa hiii imeni sikitisha sana, hivi haya maisha ya vifo vya kina mama na watoto vinavyotokea kwa uzembe wa wizara ya afya na serikali nzima vitaisha lini???
Hapa nawaletea yaliyo mkuta dada mmoja maeneo ya kaskazini mashariki mwa Tanzania na kushuhudiwa na mdau mmoja alisema hivi,,,,,

""""jaman si jambo la faragha nimemkuta mama mmoja anaumwa sana pale mt meru jaman kashikwa na uchungu na hana hata kitu manesi wanamrudisha eti akalete vifaa na anaumwa kweli ikabidi wa mama tuliokuwa pale tumsaidia hata dk kumi hazijapita kajifungua mtoto wa kike sasa nikaondoka kuja kazini kumbe hawakumchoma sindano ya kukata damu yule dada sijui ni mama kapoteza maisha nalia tena uwiiiiiiiiiiiii jaman kweli mtu anapoteza maisha kwa sindano ya 500????""""

Tutafika kweli watanzania kama hali nii mahospitalini kwetu???
Nanukuu kutoka kwa mdau mwingine aliye kasirishwa sana na uzembe huuu wa wana afya hawa na uvundo mzima wa uendeshaji na usimamiaji wa huduma za afya wa serikali yetu.

Alilonga hivi:

"""""POLE MAMA NALIA NAWEWE MPENZI. KILA SIKU NAIMBA NYIMBO ZA HABARI HIZI ZA KIPUMBAVU KUPOTEZA MAISHA YA WAMAMA NAWATOTO. ANGALIA MAGARI VIONGOZI NAWATOTO WAO WANAYODRIVE. ME NAONA TUFANYE EGYPT STYLE NCHI NZIMA KUANDAMANA. I HATE HAWA VIONGOZI BONGO. UNGEYAWEKA KWENYE MTANDAO ULIYOYAONA KWENYE HIYO HOSPITAL WAANIKWE WAJULIKANE TU.""""""

habari ndio hiyooo

No comments: