24 June 2011

MAISHA YA ADDICTION KATIKA JAMII ZETU

MAISHA YA ADDICTION KATIKA JAMII ZETU


Unywaji wa pombe upo toka zamani,unapozidi matendo yake huwa ni kinyume na tabia halisi/personality ya mtu, wote tunalifahamu hili.Ulevi ni kunywa kupita kiwango chako cha huweza kidhibiti matendo na hisia zako kwa kushindwa kuyamudu. Athari ni nyingi na mimi binafsi zimenikuta nyingi. Hapa naongelea mfumo mzima unaohusu watu wa aina yangu na wenye mtazamo kama wangu.Si maanishi kana kwamba niko sahihi bali kwa watakao soma itawasaidia,hasa marafiki na ndugu.

Lengo ni kupata ushirikiano ambao utasaidia kuniimarisha katika hatua hii ngumu ya kubadili mwenendo huu ambao niliuchukia nikiwa mdogo kutokana na mazingira niliyo kulia.Jamii naihitaji na ina nihitaji kwani nina mengi mazuri ya kuifanyia.Watu na Dini kama nguzo vimenifunza mengi kuhusu maisha ya uhusiano kati ya mungu na sisi binadamu na baina yetu binadamu.Wanaonifahamu watakubaliana na mimi.Kwa kujiunga na huduma ya wataalamu juu ya tiba ya mabadiliko ya tabia hii ya ulevi wa pombe, basi sioni cha kuficha kwani ni ugonjwa ambao tunao kila kona ya dunia na kwa wana jamii wenzangu mnajua ninaogelea nini.Silaumu bali natoa hali halisi na kuonyesha jinsi kuchanganyana kwetu kunavyoweza kuchangia matokeo mabaya baada ya kunywa pombe na nini kifanyike ukiwa na matatizo kama niliyoyapitia.

Ulevi ni addiction mbaya na hauna faida,ila wengine wanamudu na wengine huishia pabaya.Pia ulevi husababishwa na mambo mengi hadi kufikia kiwango cha kuwa moja ya maisha yako ya kila siku(Addiction).Ngumu kwa asiye mlevi au mtalaamu wa addictions kujua ugumu wa kujitoa na kuwa huru toka kwenye janga hili baya. Hebu jaribu kufikiria kile unachokipenda ghafla unambiwa ukiache haraka.Bila kujiuliza na kutambua faida na hasara zake kwako na kwa watu wako. Ni ngumu kuelewa .Na kuacha ni lazima upate msaada(surport) toka sehemu nyingine ili uweze kujaza nafasi ya mzunguko wa maisha yako ya kila siku ambayo yalikuwa na nafasi ya kitu unachotakiwa kukiacha, iwe ni kwenye pombe, drugs, sex, kamali, wizi, umbea, majidai, uchoyo na mizizi mingine ya dhambi.

Inasikitisha sana kuona watu walio karibu sana nami wanapoteza ukaribu wao kwangu kutokana na habari za matendo yangu ambayo kwa namna moja au nyingine yamewafanya wa kose imani na mimi kwa matendo mabaya yanapofikia kiwango cha kuwahusisha na wao pia. Ni mlolongo wa matukio waliyo yasikia na hata kuyashuhudia nikiyatenda hasa nikiwa nimekunywa pombe,mengine mazuri mengine mabaya sana.Sasa tofauti utaiona pale unapofanya jema,hawabadili mwenendo wa fikra zao juu ya zuri ulilofanya.Je nao wana tatizo au?. Badala ya kukuunga mkono na kukutia moyo ndio kwanza kwa chinichini wanajaribu kukuangamiza au kukukatisha tamaa,na hata wakijaribu kukupa ushauri utawasikia wakisema kwa watu “Yule pombe tu “ au kukukatisha tamaa!,Yani kama vile huyajui nahuyaoni yao? na wala huna mpango wa kuyabadili yako? Wanasahau hawajui ulikotoka na mambo yaliyokusibu na mipango unayoipanga ili kubadili tabia inayo waathiri nyote na ambayo kati yao hawaijui iko je.hili linakera sana.Sijui hapa nani kipofu?au naona naonewa? Where is the love?

Historia ya maisha ya mwanadamu toka wakati wa mwazo imekuwa na matukio mengi ya binadamu kutofautiana kimaamuzi hadi kusababisha watu kufikia hatua mbaya katika mahusiano yao“MISUNDERSTANDING“ni sumu mbaya sana pia, mtu anaweza kukuelewa tofauti na jinsi ulivyo kutokana na habari za hapa na pale na kushindwa kukuchimba kiundani.

Ina sikitisha sana pale watu mnaposhindwa kuwa kwenye mstari mmoja juu ya jambo litakalo leta faida kati yenu, mnabakia kuishia kulaumiana nakutafuta mbaya nani.
Binadamu ni mgumu sana kumuelewa na hasa anapo kuwa msiri juu ya mambo yake ya ndani na kuamua kuishi kwa kupretend. Ni nightmare! ngumu sana. Kumjua mtu kunahitaji ukaribu, muda na uhiyari wake, imani yake kwako ili aweze kujiweka wazi maana wengine hutumia undani wako kama silaha ya kukumaliza na hasa mnapo kwaruzana.

Tunaweza kujifunza tabia za watu mbalimbali kwa haraka kama tumeshawahi kushirikiana nao katika mambo mbalimbali ya maisha na pia tukifunzwa na wataalamu wanaosomea saikolojia. Lakini bado kuna upana wa uelevu juu ya kumfahamu binadamu.Na ndio maana hadi leo hakuna anayejua mbinu ya kusoma mawazo ya mtu mwingine bila kutumia mbinu kama,lugha za mwili ,maongezi ambayo utapata habari za mtu huyo kwa kumuliza maswali ambayo nayo pia hayana uhakika wa kutoa habari fasaha au sahihi ya mtu huyo.
Sasa kinacho kera zaidi ni pale mnaposhindwa kuvumiliana na kuanza kuzarauliana na kuonana kama kinyesi hata kama hampo kwenye anga za maisha ya kila mmoja.

Balaa wanaposikia lolote juu yako watajiweka mbele ilimradi watoe ushuhuda wako kwa kadamnasi waliyopo.Sasa lengo hapo ni kukujenga au kukubomoa?
Maana pindi ukipata taarifa juu ya hili basi mfarakano ndio unazidi baina yenu.Balaa huja unapojitetea huku umepata moja mbili utawasikia”mlevi huyo”.Walevi ni watu hawafanani kila mmoja ananamna yake japo tabia zinafanana.
Kwa mwenye ufahamu huwa ananyamaza,ila wenzangu namie ngumu kufunga mabakuli yao watalonga hadi majogoo na kukupa cha kuongelea. Kwa mlevi ina mwaribu zaidi maana lazima mkikutana atalianzisha kwa kuongea rabish pia.Kama unajua uko clean kuliko mwingine basi ngoja usifiwe na uwe mfano kwake, ila kama unajijua kuwa unakasoro basi jiunge nami kwa hili kwa kufuata njia zote za msaada ili turudi kwenye mstari na kuwa na amani na uhusiano mzuri tena na watu wetu, believe me im there and stapes are doing the job japo mwanzo mgumu.

Tusisahau kwamba hizi zote ni tabia za wanadamu na asilimia kubwa kati yetu tuko hivi kwani bila kujichanganya mawasilianano hayatakuwepo.Kwenye mawasiliano lazima kutakuwa na mikwaruzano ambayo inaweza kusababishwa na vyanzo vingi vinavyo weza kuepukika vikiwemo ulevi,dharau,jinsia, hisia(mapenzi) stress za maisha na mengineyo.Kama kweli unampenda rafiki, jamaa au ndugu yako jaribu
usikate tamaa kumsaidia hata kama ni mbishi ujue nae anakujaji pia, wote tunaishi kwa kujifunza na watu wanabadilika na siamini kwamba kuna aliye.Msafi japo anaweza kuwa sahihi.

Ukiona yamekuzidi huyawezi basi achana naye asije akakufanya ukawa kama yeye. Usijaribu kuwa mnafiki kwa kuwa karibu yake na kumletea stress zaidi.Hii itasaidia pande zote maana kama hamdaiani uhai katika maisha basi bora ujiweke salama kiakili na kuwa mfano bora kwa jamii. Kuachana naye hakuta kuathiri kimaisha kama ukikubaliana na uamuzi wako juu ya mwenendo wake.basi kila mtu aangalie upande wake na pindi mabadilikiko yakitokea basi angalia tena nafasi yake kwako na uwe mkweli juu ya uamuzi uliouchukua juu yake.Wengi wenye upendo wakweli kwako hawata kuacha na itauma na kumfanya achague njia bora pia ya kujirekebisha.

Kila binadamu ana wakati wake kimaisha katika kushinda na hata kushindwa, Na wote tuna fikra zenye upeo na karama tofauti japo tunaweza kuwa na mwelekeo mmoja ktk kufanya jambo Fulani na kuishia kugawanyika haimanishi tuko sawa. Kutofautiana kupo ila sababu zake ndio muhimu kuzifanyia kazi.Ukiweza Kuzijua basi zifanyie kazi kisha jaribu kuweka mazingira sawa.Tupeane nguvu ili tuishi kwa amani.

Pole sana kwa wote mlioathirika mnao athirika na tabia hii tuwe pamoja nanajua mko nami na kwa wale msiojua maana ya kuwa addicted basi mnaweza kuona matokeo yake hasa katika jamii zetu si utani athari zipo na inatisha.Mambambano yanaendelea.

PEACE

No comments: