20 June 2011

MENGI YASIYO TATULIWA

WHY?

Na Edward Hunga;

Maishani binadamu tunaishi kwa kuacumulate mifumo mingi ya maisha, na yote haya ni kwa sababu ya kuishi katika mazingira yenye kila aina ya watu wenye asili tofauti.Tamaa, Unafiki, roho mbaya na wivu na mengine mengi ni moja ya matendo na hisia zinazo tufanya tuendelee au tusiendelee.

We all know why we are here for, living as humans can be a very hard task to keep it on going. Killers and survivors always playing a cat and mouse game, shame!!

Kila binadamu hujiamini kutokana na upeo wa uelevu wake katika maisha anayo yapitia. Ila kuna baadhi ya mifumo mengine inaweza kumchanganya mwanadamu kutotambua afanyayo. Mifumo hii hutawaliwa sana na kitu kikubwa sana yaani pesa aka ngawira,michuzi, mapene, n.k. Kifupi pesa ni noma sana maana kila kitu unachotaka au kuhitaji ili uishi kina husisha pesa, binadamu tunapelekwa mbio sana na jamaa huyu. We hebu angalia jinsi unavyo hangaika kuitafuta na vikwazo unavyopata vyote vimelenga kukurudisha nyuma na kupunguza kasi ya kuzipata hizo pesa.Ukiangalia kwa haraka haraka taswira hii ya maisha ya sasa utaona wazi kabisa kwamba “mfumo wa mzunguko wa pesa” hauko fair yaani hauna uwiano kabisa, hapa namaanisha (heshima) toka juu hadi chini ya wasiojiweza

IMF hadi kwa Yule mwanakijiji wa kule kwenye mpambano wa maji na chakula na magojwa ambako vifo vya watoto ni kama breakfast kwa matajiri fulani ..ambao kwa nyazifa zao wengine wamejitahidi kubadilisha hali hii na wengine hawana hata habari.Nani alaumiwe?na je kama tunajua tatizo liko wapi ,tunaweza kupewa nafasi ya kutatua? au tutapewa nafasi ya kunyamazishwa?.Wanasema “kama huwezi kushindana nao jiunge nao!? Sasa utaungana nao vipi wakati wanachagua wa kuungana nao? Na ukitafuta mbinu za kuungana nao, wao tayari wamesha jua jinsi ya kukubana.Noma, tuna rudi palepale kwenye mzunguko wa mifumo ya maisha ya binadamu toka Enzi na Enzi.

Duh kweli mengi bado ya kuyatatua.

No comments: