13 April 2013

Mbowe afunguka juu ya tuhuma za CCM kwa CHADEMA juu ya Ugaidi

Baada ya hotuba iliyosimama juzi bungeni, Mh Mbowe amesema haya dakika chache zilizopita kwenye ufunguzi wa CHADEMA Kanda ya Dar es salaam kwenye Plaza Hotel: 
1. CCM walianza kusema Chadema ni chama cha Mbowe, mara cha Kaskazini, mara cha Ukatoliki, mara cha Wakristo na sasa wanasema ni Chama cha Magaidi

2. Anasema tatizo la udini hapa nchini limeenezwa na Kikwete na hakuna haja ya kumumunya maneno. Anasema wanavijua vikundi vilivyopata hela toka Ikulu ili kuzunguka nchi nzima kueneza udini na muda si mrefu watavitaja kwa majina.

3. Anasema pinda hafai kuwa Waziri Mkuu kwani ameunda tume ya kuchunguza tatizo la kufeli wakati tayari ana ripoti ya tume kama hiyo iliyoundwa mwaka jana.

4. Anaomba asimzungumzie Mwigulu kwani sio saizi yake na yeye kama M/kiti wa Taifa hawezi kumzungumzia mtu mjinga kama mwigulu.

Amesema ni historia kwa watu kuingia katika mkutano wa Chama kwa kulipa kiiingilio.....Kazi inaendelea
Source:Chademauk

No comments: