Leo katika angalia angalia mtandaoni nimekutana na mada anayozungumzia swala la ugaidi pale Tanzania.Mada hii iliwakilishwa na Mwana ChademaUK.Kwa mtazamo wangu niliamua kuhepa kidogo undani na mantiki ya habari yenyewe na kujaribu kuchangia kwa mtazamo wa Juu juu wa hali ya uongozi Kwetu Tanzania .....
Mada iliandikwa hivi:
Sakata la suala la ugaidi na mipango ya utekaji,utesaji na mauaji yanayotokea hapa nchini yamechukua sura mpya bungeni baada ya mmoja wa wabunge kulieleza bunge kuwa ana ushahidi wa kutosha juu ya mipango na utekelezaji wake unaofanywa na kundi la baadhi ya wanasiasa kwa manufaa yao binafsi.
Hata hivyo mbunge huyo alipingwa vikali kwa kuwa kwa nyakati tofauti tofauti alikuwa amekuwa akifanya mawasiliano na wanaotuhumiwa kuhusika na maswala hayo ya kigaidi kwa muda mrefu sana huku wakati mwingine akiwalipa fedha hivyo kuonekana kwamba anashirikiana na magaidi. Tazama Video hapo chini;
http://youtu.be/HIdFJn228Yo
Maoni yangu yalikuwa hivi:
Inategemea na kiongozi....vyama ni majina tu..Katiba na utendaji wa kujali matakwa ya wananchi ndio swala muhimu...ila kama hakuna maendeleo kutokana na mfumo wa KIGAIDI na UFISADI...ambao unajengwa na asili ya tamaa ya sisi wenyewe ndani yetu ...basi WOTE NI MAGAIDI...tu.
Majibu toka ChademaUK ni Haya:
Nakubaliana na point yako kwamba ni tamaa ya sisi wenyewe ndani yetu ambayo haileti maendeleo kwa jamii kwa ujumla. Hata hivyo nikukumbushe tu kwamba culture hii iliyojengeka ndani yetu imetokana na mfumo tuliyokulia. Umewafundisha wengi kujali matumbo yao na kujilimbikizia mali kwa njia zisizo halali kama vile rushwa na matumizi mabaya ya ofisi. Hii tabia ya kuwa Mungu mtu unapopewa nafasi ya kuongoza na kuituimia vibaya dhamana uliyopewa ni hatari kwa maendeleo. Kwa sababu hiyo ni muhimu watanzania ambao tumeliona hilo kama wewe mwenyewe Hungaz tutafute mbinu ili kubadili hali hii. Na kwa maana hiyo njia ni kubadili mfumo na kuwapa wananchi nguvu zaidi katika maamuzi mbali mbali. Hivyo viongozi wanakuwa responsible na accountable zaidi kwa wananchi. Sasa baada ya kusema hayo nina hakika kwamba CCM haiko tayari kuleta mageuzi haya ya kifikra. Japokuwa simaanishi kila aliyeko CDM ni kiongozi msafi, ni muhimu tukatambua kwamba changamoto ya kubadili fikra za watu ili kubadili mfumo zimeanzishwa na zinapigiwa kelele na CDM
Namalizia kwa hili:
Mabadiliko ya nchi yetu yana hitaji wazalendo,nikimaanisha watu wenye uchungu na wenye uaminifu kwenye utekelezaji wa mahitaji muhimu kwa Mtanzania wa hali ya chini ilikujenga msingi wa tabia hiyo hiyo ya uaminifu toka chini hadi ngazi za juu za uongozi."Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" watu hawa wa chini wanajifunza mengi kutoka kwa viongozi na siku wakipata nafasi ya uongozi unadhani hawatakuwa MAFISADI au MAGAIDI?.Keki ya Taifa(Mali Asili) ni tamu kwa kila Mtanzania na huwa tamu zaidi kwa mafisadi ambao tayari wameshaionja mara nyingi na hasa ikiwa iko mikononi mwao.Balaa litakuja tu pale wale watawaliwa ambao wanaujua mjumuiko wa viungo vilivyoitengenezakeki hiyo wanapotaka kuionja au kuimiliki.Nilazima kutakuwa na machafuko kisiasa na hata kiutamaduni na kiuchumi.Sasa muda ndio huu tuungane kama Watanzania kifikra na sio wachama fulani kwa kujumuika pamoja kutengeneza mtazamo bayana wa Katiba itakoyo linda maslahi ya Mtanzania na hasa wa hali ya chini.Wakoloni wamerudi ila kwa staili nyingine na kama hatuta beba swala hili kwenye mbereko zetu vichwani basi ni bora tulisahau swala la Haki kwa wasiojiweza...Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Kwa habarizaidi ya angalia www.chademauk.org.uk

No comments:
Post a Comment