25 March 2013

KAJALA AOKOLEWA NA WASANII WENZAKE WA BONGO MOVIE

KAJALA MASANJA
Taarifa tulizopata hivi punde Kuhusu kesi ya mwana dada muigizaji wa bongo movie anayejulikana kwa jina la Kajala aponea kwenda jela kwa miaka mitano baada ya kesi mbili zilizokuwa zinamkabili kuhitimu hukumu yake.Moja ya kesi ni .Kajala Masanja na mumewe, Faraji Augustine ambao wote waalikuwa nyuma ya nondo katika Gereza la Segerea,.Kufuatia kesi iliyowakabili ya kughushi hati na kuuza nyumba iliyo kwenye pingamizi.
Taarifa toka kwa vyombo vya habari zina sema hivi:
Hukumu ya Kajala ni kwamba, Kesi ya kwanza alitakiwa kulipa faini ya Tsh millioni 5 na ya pili ni Tsh millioni 8 au kwenda jela miaka mitano. Wasanii wa bongomovie wamezichanga pesa hizo kwa harambee ambayo ilizaa matunda  baada ya rafiki yake wa karibu  Wema na Zamaradi  na wengine kuhenya na  ATMs kukusanya pesa hizo .Kajala alitoka huru na kufarijiwa na washabiki wa bongo movie wakiongozwa na Wema Sepetu kwa habari zaidi angalia www.bongomovietz.com
Kajala akilia kwa faraja huku akipundia mashabiki na wadau hukuWema Sepetu akimkumbatia na kumsindikiza.Pole sana dada ila nadhani umejifunza mengi. jipange na uendeleze makamuzi kama kawa.

No comments: