Showing posts with label HABARI TZ. Show all posts
Showing posts with label HABARI TZ. Show all posts

17 January 2013

SERIKALI YA BARIKI FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13

Taarifa kwa Vyombo Habari:
     17-Januari 2013
 
Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Baraza la Sanaa
la Taifa, limebariki kufanyika kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii
Tanzania 2012/13 baada ya kuridhishwa na maandalizi yaliyo fanywa na
Miss Tourism Tanzania Organisation waandaaji wenye dhima ya kikomo ya
kuandaa na kuendesha mashindano hayo kitaifa na kimataifa, pia kwa
kuzingatia sheria za nchi, kanuni na Taratibu za mashindano.
Serikali pia imeridhishwa na jinsi Fainali za ngazi za mikoa na kanda
zilivyofanyika kwa mafanikio,ambapo kila mkoa umepata washindi wenye
sifa za kuwakilisha mkoa husika katika Fainali za Taifa mwaka
huu,ambapo jumla ya warembo 60 waingia rasmi kambini kesho katika
hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, kuanza mbio za kuwania Taji
hilo la Taifa.
Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika
mashindano mbalimbali ya Dunia yakiwemo ya International Miss Tourism
World, Miss Tourism United Nation, Miss Heritage World, Miss Tourism
University World, Miss Globe International n.k
Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya
Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss
Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism
Model Of The World 2008-Personality n.k
Fainali za Taifa mwaka huu zimepangwa kufanyika wiki ya kwanza ya
Februari ,wilaya ya Temeke na mkoa wa Dar es Salaam ukiwa umepewa
heshima ya kuwa wenyeji wa Fainali hizo.
Asante,
Erasto Gideon Chipungahelo
Rais

                  

                   

17 January 2011

BAADA YA KIMBEMBE CHA DC WAZIRI MKUU ATATUA MGOGORO WA UDOM

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na wanachuo wanaochukua fani ya utabibu katika Chuo Kikuu cha Dodoma alipotembelea chuoni hapo kusikiliza matatizo yanayowakabili na kuyapatia ufumbuzi
Baada ya mkuu wa wilaya ya Dodoma  kuwekwa chini ya ulinzi na wanafunzi wa chuo hicho,Waziri mkuu Mh Mizengo Pinda alitia timu jana na kuweka sawa utata uliokuwa unakikabili chuo hicho.Wahadhiri ambao waligoma kwa kutetea maslahi yao wanatarajia kuanza masomo leo.Kutokana na taarifa toka ktk ofisi ya waziri mkuu,Madai ya wahadhiri hao ambayo mojawapo ni kulipwa malipo ya posho zao, Yaliahidiwa kutekelezwa na ofisi hiyo punde mwezi Februari 2011.Mbali na hayo ofisi hiyo itamuagiza Mkaguzi mkuu wa mahesabu wa serikali(CAG) kuchunguza swala la jinsi mahera hayo yalivyo tumika chuoni hapo.

TAARIFA TOKA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA

Akizungumza na wanajumuiya ya wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) jana mchana kwenye ukumbi wa Chimwaga, Waziri Mkuu alisema matatizo yaliyojitokeza katika chuo hicho ni mlundikano wa mambo ambayo yamekuwepo siku nyingi lakini mengi ni ya kiutendaji tu na yanaweza kuisha bila kupoteza muda mwingi.

“Nimeongea na viongozi wa UDOMASA na kuwaahidi kuwa madai yenu ya posho yanaweza kukamilika mwezi Februari, nilitaka yaishe mwezi huu lakini kwa taratibu za HAZINA sasa hivi wameshaanza kushughulikia mishahara ya Januari kwa hiyo marekebisho yenu hayawezi kuwahi…wameniahidi mwezi ujao yatakamilika”, alisema huku akishangiliwa.

Amesema amemwita Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aje kukagua taarifa za mahesabu ya chuo hicho ili kubaini tuhuma zilizojitokeza za watu kulipwa hundi mbili za mishahara,walioacha kazi kuendelea kuwemo kwenye payroll ya mishahara, na wengine kukosekana kabisa kwenye payroll.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba CAG atakuwa hapa kesho… mpeni ushirikiano ili aifanye kazi kwa urahisi…, nia yetu ni kuangalia mfumo mzima wa fedha na utawala ukoje ili ikibidi uweze kurekebishwa,”alisema.

Kuhusu madai ya wanafunzi ya tatizo la maji, Waziri Mkuu alisema amemwagiza Naibu Katibu Mkuu (Fedha) Bw. John Haule ambaye alikuwepo katika ukumbi wa Chimwaga afuatilie uhamisho wa ndani wa fedha (reallocation) katika Wizara ya Maji ili zipatikane sh. bilioni 1.66 zinazohitajiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dodoma (DUWASA) kuchimba visima maeneo ya Ng’ong’ona na Ihumwa ikiwa ni pamoja na kutandaza mabomba hadi chuoni ili kupunguza shida ya maji haraka iwezekanavyo.

Pia alisema katika mipango ya muda mrefu, DUWASA pia wanataraji kupata dola za Marekani milioni 26 ambazo zitatumika kuchimba visima vingine na kujenga matanki yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 12 za maji na hivyo kuondoa kabisa tatizo la maji chuoni hapo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idris Kikula alimweleza Waziri Mkuu kwamba mahitaji halisi ya maji chuoni hapo ni lita milioni 3.5 kwa siku ambazo kati ya hizo, lita milioni 1.5 ni kwa matumizi ya wanafunzi peke yao na lita nyingine milioni mbili ni kwa matumizi ya ujenzi wa majengo unaoendelea chuoni hapo.

Mapema akizungumza na Kamati ya Makatibu Wakuu iliyoundwa na Katibu Mkuu Kiongozi, mara baada ya kuwasili mjini Dodoma jana asubuhi, Waziri Mkuu alielezwa kwamba kuna matatizo ya malipo ya posho na mishahara kwa watumishi na wahadhiri wa chuo hicho.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Bw. Idd Mwerange alimwahidi Waziri Mkuu kwamba watarudi madarasani wakati wakisubiri madai yao yakamilishwe bali aliomba kuwe na uwakilishi wa UDOMASA katika timu ya watu watakaonana na CAG.

Akifunga mkutano huo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idris Kikula alimwahidi Waziri Mkuu kwamba maagizo yake yatafuatiliwa na kwamba kesho (Jumatatu) menejimenti, idara ya Uhasibu na UDOMASA watakutana ili kuunda timu ya pamoja ambayo itakaa na kubainisha stahili za walimu wote ili orodha hiyo iwasilishwe kwa Waziri Mkuu mapema iwezekanavyo kwa ufuatiliaji.

Katika ziara yake ya jana, Mh. Waziri Mkuu alifanya vikao viwili, kimoja kikiwa cha uongozi wa Chuo Kikuu cha UDOM na kingine cha Serikali ya wanafunzi ambavyo vilidumu hadi saa 12.30 jioni na kumlazimu kuahirisha vikao viwili vilivyobaki hadi leo.

Kwa mujibu wa ratiba ya Chuo hicho,mara baada ya kukutana na serikali ya wanafunzi, Waziri Mkuu alipangiwa kukutana na jumuiya ya wanataaluma wa Chuo hicho (UDOMASA) na kisha kufanya majumuisho katika ukumbi wa Chimwaga kwa kuzihusisha pande zote tatu.

Katika vikao vyote viwili, Waziri Mkuu alielezwa matatizo yanayokibabili chuo hicho makubwa yakiwa ni uhaba wa maji, uhaba wa walimu, vifaa vya masomo na mlundikano katika mabweni.

Waziri Mkuu kabla ya kufanya mikutano hiyo miwili, alifanya ziara chuoni kukagua miundombinu ya maji safi, maji taka,vyumba vya kulala katika mabweni ya Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii pamoja na mabweni ya skuli ya Tiba na Uuguzi pamoja na ujenzi wa visima vya maji.

Chanzo:Global publishers

13 January 2011

SHEREHE ZA MIAKA 47 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kushoto) wakiwa wamesimama kupokea maandamano ya wawakilishi wa wananchi kutoka mikoa mbalimbali za Zanzibar kwa ajili ya kusherekea ya miaka 47 ya Mapinduzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima kuadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan huko Unguja jana.
Kwa taarifa kamili soma hapa: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/sherehe-za-miaka-47-ya

30 December 2010

TAARIFA YA TBC LEO TOKA TANZANIA

VIDOKEZO:
  • Wakamatwa kwa kupanga kuua na kuchukua viungo
  • Hukumu ya mbunge muuaji yatia hati hati, je niya halali??? 
  • watoto walioungana wafaulu kwenda kidato cha kwanza  




 Kwa hisani ya: http://www.kennedytz.blogspot.com/

5 December 2010

TAARIFA ZA HABARI ZA KILA SIKU PALE EAST AFRICA

KWA WADAU WANGU WOTE:
Kwa taarifa za habari katika mfumo wa video ambazo hutolewa na channel mbalimbali kama ITV,KBA,TBC CHANNEL TEN na nyinginezo mnaweza kuzipata kirahisi kwa kuangalia Blog hii http://kennedytz.blogspot.com/ jamaa anafanya kazi nzuri na amekuwa mfano mzuri  kwa wadau wanafunzi kama sisi. Tuimarishe ushikiano wa habari kwa faida ya walengwa.Pamoja sana watu wangu.