MAISHA YA UGHAIBUNI
Miaka mingi imepita toka niingie nchi ya mwingereza ambaye alikuwa mtawala wa mwisho wa Nchi yetu zama za ukoloni.Maisha ya hapa ughaibuni ni ya mnyang’anyano na hayana tofauti sana na nchi zingine hapa duniani.Kama mgeni nilifika nakuanza kujifunza jinsi ya kuishi kwa kufuata mfumo wa nchi hii.Ilikuwa ni ngumu kiasi maana kibali nilichopewa hakikuniruhusu kufanya mengi kwani kilikuwa ni cha Uwanafunzi tu. Mwanafunzi haruhusiwi kufanya kazi zaidi ya masaa 20 na kwa hali hii ikawa ngumu kukidhi mahitaji ya muhimu kama chakula malazi,mavazi na hata pango.Ni mpambano mkali si mchezo.
Nilitafuta kazi na kupata za vibarua tuu maana sikuwa na elimu wala uzoefu wa kutosha kuajiliwa kama mfanyakazi wa kudumu,mbali na hayo Uwanafunzi na uraia wa nje katu havikuwashawishi waajiri kutoa ajira.Sasa basi, kilichofuata ni mpango wa kuongeza kipato ili kukabiliana na hali Ya maisha ya hapa.Baadhi ya wenzangu waliweza kumudu kwani walikuja kwa njia ya serikali na wengine walilipiwa na wazazi wao ambao walikuwa na nyazifa kubwa na pesa nyingi nyumbani Tanzania .Mpango wa kwanza ulikuwa nikutafuta kazi mbili na kufanya masaa 20 kila moja ili kupata masaa 40 kwa wiki ambayo yangelingana sawa na kipato cha mfanya kazi wa kudumu wa kiwango cha chini. Hali hii ilihatarisha sana kibali cha kuishi nchini maana kama ukigundulika na vyombo vya dola kwa kuvunja sheria ya masaa 20 basi safari ya kurudishwa nchini kwako inakuwa imeiva.Sasa utata uja pale unapotaka kujisomesha ...elimu sio bure inahitaji ada na muda ,kama unafanyakazi muda wa masaa 40 kwa week ilikukidhi mahitaji ya msingi unapatawapi muda wa kusoma full time????.......Fuatilia habari hiii hapo baadae..kwa wale wenye maoni ya kumsaidia mdau huyu basi nitumie email hapa hungazblog@gmail.com ilitumsaidie mdau huyu.
Showing posts with label MAISHA YA UGHAIBUNI. Show all posts
Showing posts with label MAISHA YA UGHAIBUNI. Show all posts
28 October 2012
17 September 2012
MABADILIKO YA KIUCHUMI YAONGEZA MAUMIVU KWA WAGENI UK
Kutokana na mchafuko wa kiuchumi duniani na hasa hapa Uingereza, kumechangia sana maisha ya sisi tuishio huku kukumbwa na ukata wa hali ya juu.Inatambulika vilivyo kwani kwa sasa kama huna kazi ya uhakika yaani ya moja kwa moja basi kuyumba kimfuko kutakuandama tu.Kazi za vibaru zilizo kuwa zikitolewa na ma wakala wa ajira zimepeperuka na zile za kuajiliwa moja kwa moja ndio balaaa kabisa.Kutokana na hali hii ubaguzi wa kuajiriwa umeongezeka sana na kusababisha sisi wageni kupewa nafasi chache za ajira hata kama unauzoefu wa kazi hiyo.
Kwa taarifa ya undani juu ya swala hili soma makala ijayo imbayo hungaz tunaifainyia utafiti na kuweka swala hili kwenye mtazamo wa elimisho kwa wanaohitaji kujua maisha yetu hapa ughaibuni.
Kwa taarifa ya undani juu ya swala hili soma makala ijayo imbayo hungaz tunaifainyia utafiti na kuweka swala hili kwenye mtazamo wa elimisho kwa wanaohitaji kujua maisha yetu hapa ughaibuni.
23 July 2010
TOKA TANZANIA HADI UK
Ndugu wana blog leo nilipata nafasi ya kuongea na watu mbalimbali waishio hapa United Kingdom.Katika maongezi ya kawaida tu niliweza kuuliza maswali machache yanayo husu maisha yetu watanzania tuishio huku na Uraia wa nchi mbili utasaida waghaibuni kwa jinsi gani.Kila mtu alitoa majibu na maoni yake,Nilijaribu kuyachambua majibu na maoni hayo na kuafikia mtazamo wangu kama ifuatavyo;
Tulio wengi tulikuja kwa njia halali japo katika njia hizo nyingi zilihusisha mbinu mbalimbali za kiusanii kama unavyojua"bhatoto bha mujini".Kwa wanao kumbuka jinsi ilivyokuwa vigumu kusafiri kuja nchi za nje wakati wa uongozi wa mzee mchonga miaka ya toka uhuru hadi 80's.Ilikuwa ni lazima uwe una kuja masomoni na sponsor ilikuwa ni serikali,au uje kwa ajili ya matibabu au kwa shughuli za kidini na kikazi.Kipindi cha badiliko kilipotokea pale Uongozi wa Rais wetu mstaafu A.H.Mwinyi kuingia madarakani,na migogoro ya mfumo wa vyama vingi kilisababisha watu wa kila kiwango kutiririka kama maji ya mto yaingiapo baharini.Sasa basi baada ya kufika huku na kukuta mambo tofauti na fikra na matarajio yetu? maisha yetu yamukuaje? na tumeathirika au fufanikiwa kwa kiasi gani?? Habari zaidi zinakuja ila kwa sasa unaweza kuchangia ili nitakapo wakilisha habari nzima kila msomaji atakuwa ameridhika na mtazamo wa hungaz.so uliza swali au toa maoni yako hapo chini. asanteni
PIA TUPIA MTAZAMO WAKO JUU YA URAIA WA NCHI MBILI NA JE PASSPORTS HIZI ZINA MSUKUMO GANI WA MAENDELEO YA WAGHAIBUNI??
Angalia Mh Balozi Membe na balozi wa Tanzania Uk akilizungumzia swala hili
Ukiziangalia pass hizi kwa haraka haraka utazitofaulisha kwa rangi,kati ya nyekundu(UK) na kijani (TANZANIA).Kiundani tofauti ni kubwa mno hasa kwa wakazi wa hapa wenye asili ya kwetu TZ.Kwa mtazano wangu wa haraka haraka naona tofati na faida zake ni katika "USALAMA WA RAIA na"UCHUMI WA RAIA" i.e "citizen's security" and "citizen's finacial surport".Ila huu ni mtazamo wangu tu ki muhtasari mengi yapo kwenu kwa hiyo tuelimishane bila aibu kwa kuongea ukweli kwani muda wa kupretend haupo tena sasa, Ni bora kuelimishana mapema maana bado kuna watu wanafikra ambazo bila kusaidiwa wana weza kutumbukia kwenye dimbwi la msemo wa "BORA KUZALIWA PAKA ULAYA KULIKO BINADAMU AFRICA(TZ)na kusahau kabisa msemo mwingine wa "MKATAA KWAO NI MTUMWA"....changia .Nadhani wote mnao safiri kwa maborder ya nchi mbalimbali za ulimengu, mnaweza kukubaliana nami juu ya uchambuzi na utengwanishaji wa Raia wa nchi tofauti unavyokuwa kama "chuya zinavyo pembuliwa kutoka mwenye mchele"na hasa ukiingia kwenye UK borders. !!!!!!!!!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)

