27 August 2010

IMANI POTOFU HUSAIDIA MALARIA KUTUMALIZA

Tatizo la imani ya Ushirikina ama Uchawi  limekuwa kubwa sana katika kuchangia vifo vya watu wengi BARANI AFRICA na hasa kusini mwa jangwa la SAHARA.Kutokana na kutokupata elimu ya kutosha juu ya maswala ya afya watu wengi wamekuwa wakirudi nyuma kwa kuzikumbatia fikra za maadili ya kishirikina,Swala hili limesaidia kupoteza vifo vya watu wengi na hasa WATOTO.Sasa jamani vyombo vya serikali na mashirika binafsi NGOZ yanajitahidi kwa hali na mali ili kupunguza maafa haya, Tukiwa kama watanzania na Waafrika tusaidiane kuelimisha jamii zetu kwa kuwapa ushirikiano na msaada kifedha na elimu pia.Tutumie vipaji vyetu, iwe kuchora,Kuimba na hata Tekinolojia mpya tunazo pata huku UGHAIBUNI, kwani naamini kwanamna moja amanyingine mawasiliano yetu na wenzetu pale NYUMBANI hayana tofauti na jitihada zifanywazo na wafanyabiashara waki Tanzania .Kwa mfanya biashara wa kimataifa lazima ujihusishe na UNGIZAJI na UTOAJI (Importing&Exporting) kwa malengo ya kuendelea na kufungua mipaka ili upate mafanikio makubwa.Hivyo basi kama ulivyoona jinsi PROFESSOR JAY anavyo wakilisha hapo juu ,wasanii wengine pia wamejitoa muhanga na kuliwakilisha swala la TIBA Juu ya MALARIA.Leo nawalete video ya IGIZO ambalo lime HATIKIWA na Mtangazaji maarufu Bw.JULIAS NYAISANGA.Angalia ujumbe huu kisha fikiri juu ya hatu za muhimu kusaidia mpambano huu. Karibu sana. (Video kwa hisani ya ACT).



Ningependa kuwafahamu waigizaji washiriki wote wa igizo hili,Kama una wafahamu basi wasiliana nami kupitia email yangu; hungazblog@gmail.com au acha comments zako kisha nitalifuatilia swala hili asante kwa kushirikiana nasi.

WASANII WALIJIUNGA NA BI KIDUDE(LEGEND) KUHAMASISHA;


No comments: