3 January 2011

ESTA ABAKWA NA BABA YAKE? !!!!!

Na Fredrick Bundala
Mwanza.Tanzania

Miongoni mwa sababu zinazosababisha ongezeko la watoto wa mitaani ni pamoja na unyanyasaji wanaokumbana nao. Watoto wengi wanapojikuta wakipata mateso ama vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa wazazi, walezi ama ndugu zao, kimbilio lao kubwa huwa ni mtaani ambako huko huona ni afadhali kuliko nyumbani walikotoka. Wimbo huu uitwao Esta unamzungumzika binti ambaye alijikuta katika maisha ya magumu ya kunyanyaswa, kubakwa na vipigo kutoka kwa Baba yake wa kambo. Esta ni story ya kubuni ambayo kwa kiasi kidogo imetokana na historia ya ukweli ya binti ambaye ni jirani yangu. Binti huyu anaishi na Baba wa kambo ambaye mara nyingi humpiga na kujaribu kumbaka mara kwa mara bila mafanikio. Kitendo hicho kimemfanya kila siku alale na suruali ili kujilinda asibakwe. Lengo la wimbo huu ni kuwakumbusha watanzania kuwa jukumu la kuzuia unyanyasaji wa watoto majumbani linapaswa liwe la kila mmoja mwenye nafasi ya kufanya jambo la kusaidia. Wimbo huu nimeproduce mwenyewe. Thanks.
 
Sikiliza Esta hapo chini:
 Skywalker


Mradi wa AMANI  wa pale Arusha unatukumbusha kidogo nini cha kufanya kwa watoto walioathirika na Unyanyasaji huo.Pata picha hapo chini.Hungaz tuna kushukurusana mdau wetu Bw Fredrick Bundala kwa kututumia habari hii na Muziki pia.THAX
 

No comments: