29 January 2011

MASISTA FEKI WAKAMATWA MANILA-PHILLIPINES

Masista Feki

Wanawake sita walishikiliwa katika Uwanja wa ndege wa Manila wakitaka kutoka kwenda Lebanon kijanja.Baada ya kugundulika kutaka kingia nchini Lebanon kiujanja ,.huku wakiwa wamevalia kama masista(Nuns) Style hii iliokuwa na lengo la kukwepa amri iliyotolewa na Immigration (serikali) ya Phillipines kwa raia waendao Lebanon kwa nia ya kufanya kazi huko.Mbali na amri hiyo bado Wafilipino wamekuwa wakikimbilia huko kwa ajiri ya kujipatia ajira kinyume cha sheriaWanawake hao waloijifanya kana kwamba wanaelekea Hong Kong kwa ajili ya semina ya kidini walijiharibia baada ya tabia zao na jinsi walivyo tinga viwalo hivyo kutokuwa sahihi kitu ambacho kiliwastua maafisa wa Uhamiaji wa Manila.Walipo ulizwa kwa muda walikubali kuwa wanaelekea Lebanon badala ya Hong kong, kufanya kazi kama wafanya kazi wa majumbani. 
Philippines  imewakataza raia wake kwenda Lebanon tangu mwaka 2007 kwa ajili ya usalama wao.
Msala wa kustukiwa ulianza pale mmoja wao ambaye alichemka kwa kutinga viatu vyekundu na kubeba begi la mkononi  lenye marangi kibao ya kushaini na huku kavaa kanzu za kisister kwa makosa aliongeza kusema mmoja wa maafisa uhamiaji.Wapelelezi wako kazini kumtafuta jamaa aliye wapa mchongo huo maana wananchi hao wamekuwa wakifundishwa mbinu mabalimbali za kukimbilia nchi za jirani kwa ajili ya kutafuta mkate wao wa kila siku.

No comments: