17 January 2011

MKUU WA WILAYA AWEKWA CHINI YA ULINZI DODOMA UNIVERSITY

Chuo Kikuu cha Dodoma
MGOMO wa wanafunzi na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) umechukua sura mpya baada ya wanachuo hao kumteka na kumweka chini ya ulinzi kwa saa nne Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, John Tupa, wakitaka wamuone Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Tukio hili la aina yake lilitokea 15/01/11 mchana na kuvuruga hali ya usalama katika eneo hilo hivyo kumlazimisha Pinda ambaye alikuwa akifanya mazungumzo na menejimenti ya chuo hicho kuondoka kupitia njia nyingine akiwa chini ya ulinzi mkali.

Tupa aliingia katika mikono ya wanafunzi saa saba mchana katika eneo Chimwaga alipoenda chuoni hapo kufanya maandalizi ya kumpokea Waziri Mkuu Pinda ambaye wakati huo alikuwa kwenye kikao na uongozi wa chuo katika jengo la utawala lililopo umbali unaokadiriwa kuwa kilomita mbili.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, baada wanafunzi kulizingira gari la DC Tupa walitoa upepo kwenye matairi yote ya gari lake huku wakipaza sauti kuwa hawatamwachia mpaka Waziri Mkuu Pinda afike katika eneo hilo.
Kundi hilo la wanafunzi ambalo lilikuwa likitoa vitisho kwa Tupa lilimfanya dereva wake ambaye alifanikiwa kutoka kwenye gari kukimbia na kumuacha bosi wake akiwa chini ya ulinzi wa wanachuo hao.
Awali, Pinda alipowasili chuoni hapo alipokelewa kwa shangwe na umati mkubwa wa wanafunzi wakiwa pamoja na wahadhiri.
.....endelea hapa
Chanzo:Mtandao wa mwanachi

No comments: