22 March 2011

WASANII 13 WAFARIKI KWA AJALI MBAYA INAYOTISHAA!!-POLE TANZANIA

Na Dunstan Shekidele, Morogoro
WATU wapatao 13 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya katika ajali ya basi aina ya Coaster lenye namba za usajili T 361 BGE lililokuwa limebeba wanamuziki wa kundi la Five Stars Modern Taarab waliokuwa wakitokea Kyela-Mbeya kueleka jijini Dar.


Waliofariki katika ajali ya Bendi ya Five Star ni pamoja na
Issa Kijoti, Omar Tolu, Haji Babu, Sheba Juma, Omar Hashim, Tizo Mgunga, Hamisa Mipango, Husna Mapande, Samir Maulid, hasan Ngereza, Rama Kinyoya, Nasoro Madenge na mcheza shoo mmoja.
Katika video hii hapo chini unaweza kumuona Issa Kijoti akiimba na wanamuziki wenzake


Pole kwa wale wote mlioathirika kwa kuangalia picha hizi.Tusisahau kwamba speed inaua na lazima tuwe makini tunapokuwa tumebeba wenzetu maana naamini kabisa kwamba familia nyingi zimeathirika kimaisha kutokana na ajali hii .Hungaz tunatoa pole kwa Familia za marehemu wote na majeruhi pia na kwa watanzania wote. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi--AMINA
Kwa taarifa kamili na picha zaidi angalia hapa
Chanzo:http://www.globalpublishers.com
Post a Comment