7 May 2011

MATUKIO YA DIASPORA mkutano wa tatu UK katika picha

Viongozi wa Vyama, serikali na Taasisi mbalimbali wameshiriki vyema leo katika Ufunguzi wa Mkutano Wa DIASPORA III ulioanza tarehe 6- 7 Mei 2011. Diaspora ya mwaka huu imekuwa na changamoto kubwa kwa wana Diaspora ambao walitaka kujua kwa undani nini ambacho kimefanyika tayari  tokea kuanzishwa kwa Diaspora ya Kwanza. Mgeni rasmi wa mkutano huu alikuwa Mh waziri wa mambo ya nje Benard Membe. Mkutano huu utaendelea tena leo na kumalizika leo tarehe 7/5/11.Kwa mujibu wa taarifa toka Urban Pulse tulizozipata kupitia kwa Mkurugenzi wake Bw. Frank Eyembe. Mambo yakikuwa hivi:


Mh waziri Membe akiwa na Jestina kabla ya mkutano


Wimbo wa taifa ukiimbwa na waudhuriaji wa mkutano huo

Mhe waziri Membe akifungua Mkutano

Mwenyekiti wa Tanz Uk Dr John Lusingu akitoa hutuba

Lulu Mengala kutoka PPF akimkabidhi MH waziri Membe zawadi kutoka PPF kwa Ubalozi wa Tanzania na Kisha kumkabidhi Balozi wetu Kallaghe

Mh Waziri Bernard membe akiwa na Baraka Baraka kutoka urban pulse akimweleza MH mambo mawili matatu
Mh Membe akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa katika wizara ya kazi, wabunge wa CUF na CCM na Balozi wa Tanzania na naibu wake

Mh Waziri Membe akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa ubalozi wa Tanzania

picha ya pamoja
Kama kawa Menu huwa haikosi..hapa waungwana wakikandamiza msosi

Post a Comment