2 April 2014

Mayor wa Kinondoni Mh Mwenda anunua magari ya thamani ya Tsh 779 milioni.

'Kinondoni tumenunua magari kumi hard top na double cabin yenye thamani ya Tshs. 779 milioni ili kuboresha huduma za Mipango miji, elimu, ustawi wa jamii, afya, mapato pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo .
Magari haya yaliyonunuliwa kwa pesa za ndani za Kinondoni yatasaidia sana kuboresha utoaji wa huduma ndani ya Manispaa yetu na pia kuongeza mapato ya Kinondoni. Ni matarajio yetu huduma zitaboreka na wananchi wataona.'

Maneno haya ni toka kwa Mayor wa Wilaya ya Kinondoni,Dar.Ujumbe huu unatoka kwa Mh Bw Yusuf Mwenda, ameuandika katika uso wake wa kitabu.Kazi zuri na hongera kwa hilo cha muhimu ni kuhakikisha yanatumika kama yalivyolengwa.

Moja ya magari kumi yaliyonunuliwa na Kinondoni ili kuboresha huduma kwa wananchi wa Kinondoni.

Mh Mwenda watatu toka kushoto akiongea na vyombo vya habari wakati wa utambulishaji wa magari hayo


No comments: