28 December 2010

HUNGAZ AWAKILISHA " MRADI WA BUFFALO TB FREE" IN SOUTH AFRICA(PHALABORWA)

Mwaka 1998 ulikuwa ni mwaka wa adventure kwangu,kwani baada ya kumaliza elimu ya secondary niliamua kufanya kitu kitakacho nitoa kimasomaso na kunipa kumbukumbu maishani.Maisha ya uswahilini nilikokuwa naishi hayakunipa chachu ya maendeleo na kwa wakati huo niliona giza katika maendeleo ya vijana wa nchi yangu,kwani vijana tulilundikana maskani na kupata vitufulani na kisha kupeana story za ndoto ya kusafiri nchi na nje.Hii ilitokana na khali mbaya ya uchumi na maendeleo kwa vijana ambao tulikuwa tumeshakuwa watu wazima na tulihitaji kutoka kwa wazazi na kwenda kuanza maisha yetu yaani kujitegemea.



Hunga na masela  wakitaa (ubungo)
tukiangalia football huku tukipiga story
za kwenda ughaibuni,
huku begi jeusi limejaa cha ARUSHA.
 Haikuwa rahisi kusafiri kihalali kwa wakati huo kwani hata pasipoti ilikuwa ni shughuli kuipata,lakini sikukata tamaa.Nilianza harakati na nikaamua kuelekea nchini SouthAfrica ambako nilikuwa na rafiki waliotangulia.Nilisafiri na rafiki yangu Frank Mayenja aka Jagwar kwa kupitia border za Tunduma,Nakonde na Beitbridge na kuingia South Africa.


Beitbridge mpakani mwa Zimbabwe na South Africa.
Vijana wengi walipoteza maisha
 kwa kukwepa maofisa wa uhamiaji
na kuruka seng'enge ambazo zilikuwa na umeme.
 Harakati za maisha ndani ya RSA zilikuwa ngumu ila kwa Usimamizi wa Brother Mike aka Mode mambo yalikuwa mwororo.Tulifanikiwa kutambulishwa kwa Bw. LINDSEY HUNT ambaye alikuwa ni mmiliki wa kampuni ya uwindaji ya HUNT AFRICA .Jamaa alikuwa ni mchapakazi hodari aliye kuwa na ndoto ya kuwasaidia na kuwaokoa wanyama na hasa NYATI kutoka ktk Mbuga ya KRUGER Nationalal Park iliyopo maeneo ya kaskazini kusini mwa nchi hiyo,waliokuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa TB.
Bw LINDSEY HUNT alimtuma Sister Rachel ambaye aliambatana na mwenyeji wetu Brother Mode na kutupokea toka maeneo ya PHALABORWA(Nothern province of RSA).tulifika eneo liitwalo Tzeneen ambako mradi huo wa nyati ulipangwa kuanzwa.
 
Frank(jaguar)Mayenja
ndani ya Phalaborwa
Tulianza harakati za ujezi wa Bama la Nyati hao asubuhi yake.Iilikuwa ni kazi ngumu yenye kuhitaji msuli na uvumilivu maana hali ya hewa katika eneo hilo ilikuwa Joto kali sana mchana na baridi kali usiku.Eneo hilo ambalo liko karibu na MPUMALANGA mpakani mwa Mozambique na South Africa lilikuwa mbali sana na maeneo ya makazi ya kawaida ya watu.Mike(Mode Big boss),Frank Jaguar Mayenja,Robert Benta Boqwana ,Jacker na mimi mwenyewe tulifanyakazi kama viongozi wa wananchi raia ambao walikuja kama vibarua.
Baada ya muda Bama la nyati  lilikamilika na ikafika wakati wa kuwaingiza Nyati hao..dah nomaaa "I will never forget how exited i was".sitoisahau hiku hiii.Wahungazi nimeona niwadokeze haka kastory maana najua kuna watu wanaopenda mambo ya asili na hasa wanyama.Nilijifunza mengi na kwa sasa nawasiliana na wahusika wa maliasili ili kuifanikisha ndoto yangu.
 Kwenye habari hii unaweza kuona jinsi gani Mwingereza Bw.Hunt alivyo hussle na kuitimiza ndoto yake yakuwaokoa wanyama hawa toka kwenye gonjwa la TB(Kifua kikuu). i am realy still inspired!!!".

Documentary hii fupi ilitengenezwa baada ya Hungaz kuondoka,ila unaweza kumuona Frank jaguar akiwa na Bw Hunt wakimuhudumia mtoto wa nyati. picha zaidi angalia baadaya ya video hii.


"Buffalo Warrior" - DOCUMENTARY FOR NAT GEO / ANIMAL PLANET from Bronwyn Harvey on Vimeo.


Frank Jaguar Mayenja akijipongeza baada ya mafanikio ya mradi huo,hadi sasa
Bother wangu huyu ambaye alikuwa mfanyakazi wa pale Coco Beach TZ anawakilisha kama Manager katika mradi huu
Robert Benta Boqwana (kushoto) akiwa na Brother Mike Sipho aka Mode
wakati wa ujenzi wa mwanzo wa Mradi huu;
picha za hungaz nikiwa maeneo hayo nitaziweka sooon ........

No comments: