19 December 2010

"Mtoto wa Mkulima" Alipiga Chini 'Shangingi' -

 Gharama yake TSh 280milioni, asema nchi yetu ni masikini...



Toyota Land Cruiser ya 2010 :
Gari kama hii yenye thamani ya Tsh 280 milioni(£118,ooo ) ni kashfa kwa serikali kununua magari haya kwa kila waziri,hebu piga hesabu ni kiasi gani kitatumika kuwanunulia mawaziri wote?? na hata bei yake ni changa la macho kwani mpya kwa bei inayo fahamika ni £70,000 sasa hako kajuu kako wapi au hayo yaliyo agizwa yana mbingu ndani yake??
Na je ni kiasi gani kina weza kutumika kununua AMBULANCE zilizo tumika kwa hospitali zetu..jamani eeeeeh!!!!! mi sina mengi pata habari kamili hapo chini kutoka kwenye chazo kimoja cha habari pale TZ.


Mh.Mizengo Pinda(waziri mkuu TZ)

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mtoto wa mkulima baada ya kukataa gari jipya ka kifahari alilonunuliwa na wasaidizi wake kwa akisema kwamba alilonalo linamtosha.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana jioni kwa njia ya simu, Pinda alisema kuwa uamuzi huo aliuchukua mwaka huu kabla ya uchaguzi mkuu kuanza baada ya kukataa kulitumia gari jipya aina ya Landcruiser VX 8 lenye thmamani ya sh milioni 280.
Alisema kuwa aliamua kukata kulitumia gari hilo baada ya kungundua kuwa alilonalo ambalo ni la bei ndogo kuliko hiyo bado lina uwezo.
"Ni kweli nimelikataa kulitumia gari hilo kwani niliona hata gari hili ambalo nimeanza nalo kulitumia kama mawaziri mkuu bado halikuwa na matatizo, sasa kwa nini nipewe jingine jipya, hii itakuwa ni matumizi mabaya fedha za serikali," alisema.
Alisema baada ya kulikataa kulitumia gari hilo aliwaagiza watalaam wake kwa sababu tayari walishalinunua kumtafuta mtu mwingine wa kumpa kulitumia, lakini kama angeshirikishwa katika mchakato wa awali hangewakubalia.
Pinda aliteuliwa kuwa Maziri Mkuu mwaka 2008 baada ya aliyekuwa akishika wadhifa huo, Edward Lowassa kujiuzulu kutokana na kuibuka kwa kashfa ya Richmond pamoja na mawaziri wengine ambao Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Nazir Kamaragi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Pinda ambaye anakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kukataa gari jipya alilonunuliwa kwa lengo la kubana matumizi alisema kuwa watu wanatakiwa kujua kuwa Tanzania nchi masikini sana hivyo tunahitaji kutumia vyema kipato chetu badala ya kukitumia kwa matumizi ambayo sio ya lazima.
Alisema kuwa mazoea ambayo Watanzania wajijengea kwamba viongozi wa juu wa serikali wanapenda kila mara vitu vipya na vya gharama kubwa hanapaswa kufutwa kwa vitendo.
"Hii tabia ya kufikiri kwamba gari zuri lazima liendane na hadhi ya mtu ni vyema sasa tukaiacha," alisema na kuongeza:
"Kutokana na tabia hii hata watengenezaji wa magari nao wamejua udhaifu wetu wamekuwa wakijaribu kubadilisha muundo kidogo tu na kuja na magari mpya ambayo wanayauza kwa bei kubwa".
Pinda ambaye ndiye anayetoa kibali cha ununuzi wa magari ya serikali alisema hatakubali kuidhinisha viongozi wa serikali kutaka kununua magari ya kifahari wakati wanaweza kutumia magari ya kawaida.
Hata hivyo,alisema kuwa hawezi kupiga marufuku moja moja ununuzi wa magari ya kifahari kwa vile ni jambo ambalo linahitaji kuchukuliwa kwa hatua, lakini taratibu watedaji wa serikali watahamia katika kutumia magari ya kawaida.
Waziri Mkuu ambaye akiwashukuru wabunge kwa kumwidhisha kuwa waziri mkuu alisema yeye ni mtoto wa mkulima, alisema suala la kudhibiti ununuzi wa magari ya fahari kwa viongozi wa serikali alishaalianza muda mrefu.
Mwaka jana Pinda, aliwaagiza watendaji wa serikali watafute namna ya kupunguza matumizi ya fedha za umma ikiwa ni pamoja na kutonunua magari ya kifahari. Aliwataka watendaji hao wabadilike, waache ubinafsi na wasijifikirie wao tu, kuna mamilioni ya watanzania wanaohitaji fedha kidogo zilizopo.
Katika Wizara za Serikali kuna magari mengi ya aina ya Toyota Land Cruiser VX yanayouzwa kati ya Sh 160 milioni hadi Mwaka 2008 serikali chini ya uongozi wa Pinda ilifanya marekebisho makubwa ya namna ya udhibiti wa uendeshaji wa magari ya kifahari kwa mawaziri na viongozi wengine ili kuondokana na matumizi mabaya ya mali za umma.
Ripoti ya Mpango wa Serikali kuhusu Orodha ya Magari yake na Kudhibiti Matumizi ambayo ilipendekeza pamoja na mambo mengine magari ya kifahari ya mawaziri maarufu kama mashangingi yanunuliwe kila baada ya miaka saba badala ya miwili ya wakati huo.Utaratibu uliozoeleka ni kwamba, gari la waziri huweza kununuliwa kila baada ya miaka miwili tangu linunuliwe na kuanza kutumika, kisha hutumiwa na watendaji wa ngazi ya chini, au kuuzwa au waziri 'kujiuzia'.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya serikali ya mwezi Aprili 2008 jumla ya magari yote ya serikali nchini yalibainika ni kati ya 35,000 hadi 40,000.Kati ya orodha hiyo magari ya kifahari ya Toyota Landcruiser Vx8 na VX, Gx na aina nyingine ya Landcruiser yalikuwa kati ya 10,000 hadi 15,000.Takwimu za sasa, gari moja aina Toyota VX8 linauzwa kwa sh 280 na kwamba VX la kawaida ni sh 120 milioni, huku gharama za operesheni ikiwa ni pamoja na matengenezo ya kila wiki na mafuta ni kati ya Sh moja hadi 1.5 milioni, kutegemea safari. Magari hayo 40,000 ni kuanzia Serikali Kuu na Halmashauri za Wilaya, miji, manispaa na majiji, ambayo ni pamoja na yale ya miradi maarufu kama DFP ambayo hutokana na wafadhili.
 Orodha hiyo inaonyesha sehemu kubwa ya magari hayo ni Toyota Pickup na Hard Top, ambazo zimekuwa zikitumika zaidi vijijini huku mashangingi ya Vx na Gx yakirandaranda mijini.Pendekezo la serikali ni kwamba katika ngazi ya Serikali za Mitaa, linataka Mkuu wa Mkoa pekee ndiye atumie Vx ili kuwezesha Rais anapofika aweze kulitumia huku Wakuu wa Wilaya na watendaji wengine wakitakiwa kupatiwa gari za kawaida kama Toyota Landcruiser si Vx.

Chanzo cha Habari: Gazeti la Mwananchi





No comments: