4 January 2011

CHIDI KUSHAMBILIA TOKA LUNINGANI

CHIDI BENZ
LA FAMILIA:
Ilalaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!Braaaaaah braaaaaaaaah!!

Msanii maarufu kwa kufoka foka Rashid Makwilo aka Chidi Benz anatarajiwa kutokea kwenye Luninga kama mtangazaji wa Televisheni ya East Africa TV, Channel 5. Akichonga na Bongo5 Chidi Benz alisema kimya chake cha muda mrefu hakikuwa bure bali alikuwa anajaribu kuweka mambo yake sawa ili aweze kuingia mwaka 2011 kwa kishindo cha ajabu."Nimejipanga vya kutosha katika idara zote za tasnia ya burudani kuanzia kimuziki hadi mambo mengine".
Akiendelea chidi benz alisema kwamba sasa amejipanga kurudi kwenye fani ya muziki kama msanii wa kweli kwani ana mapini ya ukweli ambayo unaweza peleka na yakasikilizwa na kupendwa mahala popote ulimwenguni na si Tanzania ama Afrika pekee.
"Nimesharekodi nyimbo za kutosha, siku si nyingi utamsikia chidi ambaye hamtomdhania."
Akichonga kuhusiana na mchakato huo wa yeye kutangaza kwenye luninga Chidi alisema kipindi chake ambacho bado hakijapewa jina ambacho kinatarajiwa kuanza kuonekana siku za karibuni kitakuwa ni maisha ya ukweli ama uhalisia kwa kifupi (Reality Show) wa maisha yake akiwa katika mishe na game ya HipHop.

Habari na Bongo 5/Wahapahapa.com

No comments: