5 January 2011

PETER ANDRE AMYANG'ANYA FRANK LAMPARD DEMU

Peter Andre  Elen Rives  na  Frank Lampard
Taarifa za hivi karibuni toka kwenye vyombo vya habari hapa uk kwamba Peter Andre, aliyekuwa Mume wa Model Kate(Jordan) amejipatia demu mpya baada ya kukaaa ubaoni bila demu kwa muda mrefu.Peter mwimbaji wa "Mysterious girl" kibao  kilichotamba miaka ya 90 walionekana wakiwa pamoja na Elen Rives ex girlfriend wa (Frank Lampard  mchezaji wa timu ya Clelsea na timu ya taifa ya England).Wapendanao hao ambao wote ni macelebrity wanafungua mwaka huku kukiwa na mfukuto kwenye mahusiano ya wapenzi wao wa zamani.Inasemekana kwamba Bi Jordan na Alex(mume wa Jordan) wanazinguana hadi kufikia kwenda kwenye holiday ili kuangalia mpango mzima wa uhusiano wao,kama waendelee au wamwagane.Kwa mwana ndinga  Lampard na ngoma yake mpya ilionekana kana kwamba kila mtu aliitaji muda wapekee kipindi cha mwisho wa mwaka na hata siku ya usiku wa mwaka mpya hawakuwa pamoja na ina semekana hakukua na makubaliano juu ya maswala fulani...Anyway yote ni maisha .
Sasa shughuli kwa bwana Peter maana ana watoto wawili na kazi ya kuuweka sawa umaarufu haitakuwa rahisi.
Peter Andre-Mysterious Girl:

No comments: