NANI ALAUMIWE???
WAWILI WAUWAWA:
Jamani kwani lazima watu wafe kwa ajili ya haki zao? sasa serikali iko madarakani kwa ajili ya kulinda na kuwatumikia raia au kuwaua?? eti TANZANIA ni nchi ya amani? kweli?..pata full habari tika kwa kamanda wa Arusha Bw Thobias Andengenye ,
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye |
Hata hivyo mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Arusha, Salash Toure akizungumza na TBC amesema amepokea miili mitatu mmoja ukiwa na majeraha ya risasi na majeruhi ishirini na tisa. Tayari miili miwili imetambuliwa.
Kamanda Andengenye amesema watu kumi na mmoja wanashikiliwa na polisi ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Wilbroad Slaa, mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na kwamba watuhumiwa wanafikishwa mahakamani hii leo mjini Arusha.
Katika maandamano hayo yaliongozwa na viongozi waandamizi wa CHADEMA polisi ililazimika kupiga mabomu na kuziba baadhi ya barabara za mji wa Arusha kwa zaidi ya saa mbili ikiwemo ile inayoelekea kituo kikuu cha polisi kufuatia baadhi ya waandamanaji kuvamia eneo hilo na kuanza kurusha mawe.
Mwandishi wa TBC Secelela Kongola aliyekuwa anafutialia tafrani ya maandamano hayo amesema purukushani za maandamano hayo zilizuruga shughuli za kawaida katika mji huo wa Arusha ambao ni maarufu kwa shughuli za utalii.
Chanzo: Sechelela Kongola, Arusha
No comments:
Post a Comment