Nembo ya kikundi cha vijana wa Kitanzania kupitia muungano wao kwenye facebook (FACEBOOK TANZANIAN GROUP) |
Katika kile kinachoonyesha kuwa Vijana nchini wanazidi kupata mwamko juu ya matatizo yenye kuwapata vijana wenzao katika sehemu mbalimbali, Wadau wa Tanzanian Group, ambao ni mjumuiko wa marafiki wenye kuunganishwa na mtandao jamii wa Facebook, waliungana na watoto waishio katika mazingira magumu wanaotunzwa katika kituo cha watoto yatima cha Ummra kilichoko Magomeni Mikumi, kusherehekea mwaka mpya pamoja nao.
Kassano Mushumbusi Jonathan, mmoja wa wasimamizi/waratibu wa kikundi hicho waliliambia Jukwaa Huru kwamba, pamoja na msaada kidogo walio peleka kituoni hapo, ikiwa ni michango toka kwa wadau walio ndani na nje ya kundi hilo, lengo lao jingine ni kujaribu kuwa karibu na vijana waishio kituoni hapo ili kuwaonyesha upendo ambao wanahisi wameukosa kwenye jamii na hivyo kujiona kama wao wana makosa.
“Tumepeleka msaada kidogo, kulingana na mwitikio wa wadau walio ndani na nje ya kundi hilo, lakini pia dhamira yetu kuu ni kwenda kukaa na vijana wale ambao kimsingi sisi tunaamini kuwa msada mkubwa wanaouhitaji ni mapenzi toka kwa vijana wenzao, na tunaamini kuwa kwa muda tutakaokaa nao tutawapa faraja kubwa kuwa wapo watu wenye kuwapenda huku mitaani licha ya kuwa hawana cha kuwasaidia kwa maana ya mali” amesema mratibu huyo.
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na kile kinachoweza kuchukuliwa kama mwelekeo chanya wa mitandao jamii mbalimbali hapa nchini, ambapo imekuwa ikikusanya vijana ambao wamekuwa wakichagua kutumia umoja wao kwa malengo ya kimaendeleo zaidi tofauti na awali ambapo wengi walikuwa wakiitumia kwa mwelekeo hasi.
Bilashaka, umefikia wakati sasa wa Watanzania zaidi na hususan vijana ambao ndio watumiaji wakuu wa mitandao hii, kuhakikisha kuwa wanatumia fursa za namna hii kwa lengo la kuunda mitandao itakayokuja kuwaletea manufaa baadae, na kwa ziara kama hizi ni moja ya mambo ambayo jamii ikiyaunga mkono basi itawapa vijana msukumo wa kutumia mitandao hii kwa manufaa ya jamii zaidi kuliko kupotezana kimila na kiutamaduni.
Zawadi mbalimbali |
misaada ya chakula na vinywaji n.k |
Watoto wa UMMRA wakifurahia na Tanzania Group |
Dada Waydaeli Josephat(TZ Group)akiwa na mmoja wa watoto |
Watoto wakiburudika kwa kucheza muziki |
Wana Tanzania Group ndani ya UMMRA |
Maana: "Mimi nimechangia kwa maskini na kukaribisha nawe pia-Tanzania Group" Unaweza kuwatembelea vijana hawa katika ukurasa wao kwa kubonyeza hapa , na kuwasiliana nao zaidi ili kujua namna ya kuwasaidia au kushirikiana nao. |
No comments:
Post a Comment