UTATA WAGUBIKA MMILIKI WA MBWA WALIVYO MTAFUNA MTOTO, KUNUNUA BAADHI YA MAJENGO YA IKULU
Na Nickson Mahundi,Ludewa.
Utata umeendelea kugubika kwa wananchi wa wilaya ya Ludewa kuhusiana na mmiliki wa Mbwa ambao walimuua mtoto Ibrahim Faraja Chipungahelo Bw.Bosco Thobias Lingalangala uhalali wa kuyanunua baadhi ya majengo ya Ikulu ndogo ya wilaya ya Ludewa na kugeuza sehemu ya kufuigia mbwa ambao ni hatari kwa maisha ya Binadamu.
Hali hiyo ya sintofahamu imeendelea kuwashangaza wananchi hao wenye shauku ya kuhoji kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa watakatembelea wilaya hiyo kuanzia sasa kutokana na miliki huyo kumiliki majengo hayo ya ikulu na kuendelea kuwatishia Bastola pindi wanapopita katika Ikulu hiyo.
Akiongea kwa jazba Bw.Kasbeth Mhagama wakati akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo la mtoto kuuawa na mbwa kisha kuliwa nyama alisema kuwa wananchi wameshangazwa na ujasili wa mtu huyo kwa majibu yake ya kejeli kwa wafiwa.
Mbwa wa aina hii bila uangalizi wanaweza kuhatarisha maisha ya mtu |
Bw.Mhagama alisema tayari Mbwa hao walikuwa wameshawala mbuzi zaidi ya 57 lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa katika hilo na mmiliki huyo amekuwa na nguvu kubwa ikiwemo ya kununua baadhi ya majengo ya ikulu hali ambayo ni hatari sana kwa wananchi.
“tunashangazwa na hali hii inayoruhusu mwananchi wa kawaida kumiliki majengo ya Ikulu na kuwatisha watu na bastora kila wakati na tunajiuliza ninani aliyoko ngazi ya juu yaani taifani anayempa kiburi hicho ambacho kinawafanya wananchi wa wilaya ya ludewa wasiishi kwa amani”,alisema Bw.Mhagama.
Alisema
Pichani:
marehemu Ibrahim akiwa na wanafamilia wakati wa uhai wake-koti la blue na Picha Ndogo pembeni
Regards
Erasto Gideon Chipungahelo
President Africa Tourism Promotion Center ,owner and Organisers of Miss Tourism Tanzania,Miss University Tourism World,World Great Safari Tour,Ant Poaching International Marathon,National Parks International Marathon,Miss Heritage World Pageant and World Tourism Awards- The Symbol Of World Heritage
No comments:
Post a Comment