10 August 2014

MKUTANO WA DIASPORA 2014

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa Ndugu Francia ambaye alikuwa mmoja wa washiriki wetu pale Serena Hotel Tanzania kwa ajili ya mkutano huo tunawakilisha taarifa fupi ya matukio ya mkutano huo uliofanyika tarehe 14 na 15 august 2014:





"Jamani Diaspora Homecoming event 2014 ilikuwa nzuri na ya mafanikio sana. Hongera kwa waandaaji Susan Mzee na Team yako. You really exceeded most people's expectations. Weldone guys. I was honored to be the Singer for the event Thank you so much.
Naomba kushare Baadhi ya Mada, najua kuna wawakilishi watakaowaambia kila kitu but nimeona kama mshiriki ningependa kuwarushia some few dondoos.

Suala la Uraia pacha bado ni la mbali na si la kutegemewa kufanikiwa hv karibuni. Rais bado anasisitiza kwamba WaTZ wa diaspora hamjalitilia mkazo na kulipigia debe enough. Liko kwenye mjadala lkn waandaaji katiba wanahitaji kupewa vigezo vya kutosha kuonyesha umuhimu wa hili swala. kumbukeni katiba inaandaliwa na wasomi wa hali ya juu hivyo kuwaface hawa watu na hoja zenu ili wabadili sheria you need to be well organised, na mna evidence za kujiback up. so more research in this area is needed esp kutoka nchi za Africa zenye uraia pacha, kusema faida na hasara kwa wanadiaspora na nchi km hii sheria itapitishwa..
Ilipendekezwa na baadhi ya watu kwamba kuwe na link moja (Website or Blog) ya wanadiaspora woooote duniani ambayo itatumiwa kutuma mapendekezo na kushare ideas na mambo mbali mbali yanayohusu WaTZ wa diaspora, at the same time kutumiwa na ofisi za diaspora Tanzania au hata watu wengine kuwasiliana nasi. This is still a suggestion.Baadhi ya watanzania wanapendekeza greencard instead of uraia pacha.
- Mada kutoka makampuni ni pamoja na Watanzania mlio nje ya nchi (whatever the nationality) mnahimizwa na kuhamasishwa kununua nyumba za National Housing zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini. Kutoka NHC wenyewe hizi nyumba ni the cheapest kulinganisha na nyumba zinazouzwa na makampuni mengine.
Kuhusu mortgage walisema kuna uwezekano wa kutumia bank za nje, however KCB TZ bank na baadhi ya bank nyingine hapa nchini zina account ya diaspora hivyo mnaweza kutumia hizi bank kupata mortgage.


Amemalizia kwa kusema:
Mambo mengine yaliyozungumziwa ni mikopo ya elimu ya juu nchini kwa wale wanaotaka watoto wao waje kusoma TZ, Sasa kuna mikopo kupitia Higher Education Students' loans Board. Hivyo kuna mikopo ya kuwasomesha watoto wenu na nyie wenyewe hapa nchini. kama unataka kusoma nje ni baadhi ya nchi tu zina mkataba e.g Quba, Ukraine na zingine nimesahau but not nchi kama UK, US.

Jamani hizi ni baadhi ya mambo mengi mno yaliyozungumzwa, swala la investments ndo limeongelewa sana na WaTZ mmehimizwa kuinvest nchini kwenu.


Je kwa mtazamo wako unalionaje swala hili? wasiliana nami kwa barua pepe ili tuifungue jamii;

Habari katika picha kwa hisani ya Ndg Francia













Greeting with President Jakaya Mrisho Kikwete at the Diaspora Event, Serena Hotel Tanzania



UK Diaspora Ladies na Issa Michuzi aka Ankal 



No comments: