30 January 2011

KARIBUNI NYOTE KWENYE IBADA YA KUWAFARIJI WAFIWA

FAMILIA YA MUBARUKU MZEE WA READING INACHUKUA FURSA YA KUWAKARIBISHA WATANZANIA POPOTE PALE LEO JIONI KUANZIA SAA KUMI NA MOJA NA NUSU ,KWENYE IBADA FUPI YA KUWAFARIJI NA KUWATIA MOYO WAFIWA ,MUBARUKU MZAZI WAKE MAUTI ILIMKUTA SIKU YA IJUMAA, HUDUMA YA IBADA ITAFANYWA KWENYE ADDRESS IFUATAYO

ADDRESS: 2 Appleshaw Court , School Rd ,READING. RG31 5AL
TEL: +44 7799435327 - UK

Ujumbe umeletwa kwa hisani ya:

Jumuiya Ya Watanzania Reading-UK
Blog :http://www.tareading.blogspot.com/
Email:tzra2009@gmail.com
Tel No: +447865673756

CCM Branch -Reading ,
Berkshire .
United Kingdom.

29 January 2011

MASISTA FEKI WAKAMATWA MANILA-PHILLIPINES

Masista Feki

Wanawake sita walishikiliwa katika Uwanja wa ndege wa Manila wakitaka kutoka kwenda Lebanon kijanja.Baada ya kugundulika kutaka kingia nchini Lebanon kiujanja ,.huku wakiwa wamevalia kama masista(Nuns) Style hii iliokuwa na lengo la kukwepa amri iliyotolewa na Immigration (serikali) ya Phillipines kwa raia waendao Lebanon kwa nia ya kufanya kazi huko.Mbali na amri hiyo bado Wafilipino wamekuwa wakikimbilia huko kwa ajiri ya kujipatia ajira kinyume cha sheriaWanawake hao waloijifanya kana kwamba wanaelekea Hong Kong kwa ajili ya semina ya kidini walijiharibia baada ya tabia zao na jinsi walivyo tinga viwalo hivyo kutokuwa sahihi kitu ambacho kiliwastua maafisa wa Uhamiaji wa Manila.Walipo ulizwa kwa muda walikubali kuwa wanaelekea Lebanon badala ya Hong kong, kufanya kazi kama wafanya kazi wa majumbani. 
Philippines  imewakataza raia wake kwenda Lebanon tangu mwaka 2007 kwa ajili ya usalama wao.
Msala wa kustukiwa ulianza pale mmoja wao ambaye alichemka kwa kutinga viatu vyekundu na kubeba begi la mkononi  lenye marangi kibao ya kushaini na huku kavaa kanzu za kisister kwa makosa aliongeza kusema mmoja wa maafisa uhamiaji.Wapelelezi wako kazini kumtafuta jamaa aliye wapa mchongo huo maana wananchi hao wamekuwa wakifundishwa mbinu mabalimbali za kukimbilia nchi za jirani kwa ajili ya kutafuta mkate wao wa kila siku.

Raw Video: Tanks roll in Cairo this Saturday morning


Cairo in Mess
 The Egyptian capital Cairo woke up to the prospect of another day of protest on Saturday, as tanks rumbled through the streets and crowds gathered once more.
Click this link to see all updates on video: http://news.yahoo.com/video/world-15749633/raw-video-tanks-roll-in-cairo-saturday-morning-24006473

Click below to watch live coverage
WATCH LIVE HERE:

ASKOFU ADAKWA NA UHAMIAJI TANZANIA

Akituhumiwa sio raia !!!!!
ASKOFU wa Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian
Fellowship, Fredrick Mukongo, amekamatwa na Idara ya Uhamiaji na
kupelekwa gerezani baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, kudai kuwa ni
raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC)......endelea hapa

28 January 2011

POLE KAKA AGREY URIO KWA KUFIWA NA NDUGU YAKO

TANZIA READING UK


Familia ya Aggrey Urio wa Reading-United Kingdom, anasikitika kuwatangazia msiba wa Mdogo wake kilichotokea  tarehe 25/01/2011 -Tanzania.

Marehemu ni mdogo : Aggrey Urio mkazi wa Reading UK

Habari za msiba huu ziwafikie watanzania wote waishio Readinge na sehemu zingine za UK na ndugu wote, jamaa na marafiki popote walipo.Mfiwa anatakiwa kusafiri na kama ilivyo desturi yetu ,basi fikisha mchango wako ili aweze kusafiri

TEL: 07853110307; 07760404352
ADDRESS: 19 BARNWOOD CLOSE ,READING. RG30 1BY

Director Of Communication
CCM Branch -Reading ,
Berkshire .
United Kingdom


Wana hungaz tulijumuika kwenda kumpa pole kaka yetu Agrey Urio mitaa ya Reading UK kwa kuondokewa na kaka yake wa familia.mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi ...Amina

Hungaz nikiwa  na bro wangu Agrey Urio siku ya kumpa pole


Hungaz nikiwa na masela eneo  la tukio

Hungaz ,chairman na denja ndani ya bongo shop


Hungaz tukitoa pole kwa bro wetu Agrey wa kwanza kushoto


25 January 2011

FROM S&S RECORDING STUDIOS-USA


S&S RECORDS is not new to hungaz,but for those who never heard them, then here they are.Been productively excellent and well organised under one of the Tanzanian hip hop legend STIGO(former Diplomats group).Have released one of their remarcable product that they have done with artists ie BEEZY(Benson Mokiwa)  featuring  Shanice Stevens and Big Z(Golden Mokiwa)aka Zigua.In this project you can hear how these guys been grown and gone real harder ,The beat is so sick as well as flows.Hear they come with the song called DANCE. click on player below to listen.

24 January 2011

TRAFFIC WAPIGWA MARUFUKU KUPOKEA RUSHWA(Kisafisha njia)-MBEYA

KAMANDA wa polisi Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amepiga marufuku kitendo cha askari wa usalama barabarani (Traffic) kuwatoza madereva Sh 9,000 kama malipo ya kusafisha njia ili wasikamatwe tena kwa makosa mbalimbali.
Kauli ya kamanda huyo, imekuja baada ya madereva wa daladala jijini Mbeya kutoa malalamiko katika mkutano baina yake na wamiliki na madereva wa jijini hapa, uliofanyika ukumbi Rayol Zambezi.

Madereva hao, walitoa kero zao katika risala yao kwamba wamekuwa wakitozwa Sh9,000 na trafiki kwa madai ya kusafisha njia na Sh1,000 kila kituo ambako wamesimama.

“Nimesikia kero zenu nyingi, lakini nasema hivi mbele yenu utaratibu wa kusafisha njia kwa Sh9,000 ukome kuanzia leo na kutoa Sh1,000 hiyo ni rushwa hivyo mambo haya yasijirudiwe tena,”alisema Kamanda Nyombi.

Nyombi alisema kitendo cha dereva au kondakta kutoa Sh1,000 ni kosa la jiani kwani mtoa rushwa na wanaopokea wote hao ni wahalifu na kwamba makondakta wamekuwa wakichochea kutoa rushwa ya Sh1,000 kwa trafiki ili kukwepa makosa ambayo wanafanya ikiwa ni pamoja na kujaza abiria na ubovu wa magari yao.
Kamanda aliwataka madereva hao, kufuata kanuni, taratibu na sheria za usalama barabarani ili kuondokana na migogoro baina yao na jeshi la polisi.
Katika hatua nyingine kwenye mkutano huo, Mchungaji William Mwamalanga alipewa bahasha ya fedha kwa kazi aliyoifanya ya kuwakutanisha madereva hao na jeshi la polisi.

“Unajua afande RPC mimi nilijua nafanya kazi hii kwa kujitolea, lakini nimeweza kupata hii bahasha nawashukuru hawa madereva kumbe unaweza ukafanya kazi na mshahara ukaupata baada ya kazi hiyo,”alisema Mchungaji huyo.

Mwananchi.co.tz
Brandy Nelson,

Mbeya

22 January 2011

BODY SCANNERS NDANI YA AIRPORT ZETU NI KUZALILISHANA? AU NI SWALA LA USALAMA

cartoonist wakituonyesha hali halisi
Kwanza samahani ndugu kwa kuweka swala hili kwa mtazamo wa picha hapo juu.Kifupi hii ndio hali halisi ya tunakoelekea au tulipo hivi sasa.Mfumo wa CCTV na Scanners umeingia hadi idara ambayo inawaumbua watu wengi na kuwafanya wasi enjoy safari zao.Kwa mtazamo wako ungependa swala hili litekelezwe katika mwelekeo gani?,maana hali ya Ugaidi (terrorism) una ongezeka. Je watu wasi sachiwe eti kisa mtu anaogopa kuonwa nani hii zake??.Hapo ndipo penye utata.Je kwa watu wadini mnalionaje swala hili???

Hali halisi ktk airpot moja ughaibuni
Niliweza kumpata rafiki yangu msichana wa kati ya miaka 26-29 ambaye alikuwa anataka kusafiri ila swala hili lili mtiasana wasiwasi..niliongea naye kwa muda mrefu na kwakweli sikuweza kumridhisha kwa majibu yangu ambayo mtazamo wake ulikuwa ni wa kubunibuni tu.

Alisema hivi:--"I am due to be flying in about a month's time. I really really detest the idea of this whole human body scan thing where any odd person can view my private parts and genitals. Most men don't seem to think it is a big deal, but as a woman it is a hell of a big deal to me. I do not have anything to hide, but at the same time I dont to be displaying my nude self to any old pervert sitting there (people can argue it is their job, it is for our safety etc etc but ultimately, it boils down to a stranger is seeing virtual images of my breasts, vagina, bottom etc which I am NOT comfortable about irrespective of any argument anyone can give me) Even today on the news there is a situation of an employee used the machine at the airport I am due to fly from to oogle one of his female co-workers"


Akaniuliza hivi; - Do I have any rights at all in terms of choosing to not go through this? Can I refuse? And if I do, will I be submitted to more humiliation or decline my boarding? Or basically has the government taken away my human rights and submitted me to being some cheap 30 second strip dance routine for the oogling eyes at the security staff at the airport??

21 January 2011

KANUMBA KUJA NA NGUVU MPYA 2011--YUKO USA AKIJINOA

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Steven Kanumba(The greatest) ameamua kufanya kweli mwaka huu.Msanii huyo ambaye kwa sasa yuko mapumzikoni nchini Marekani amefafanua kwamba anajiandaa na makamuzi ya kufa mtu mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata kupitia libeneke lake zina kamilisha habari hii kwa kuonyesha picha za shooping ya baadhi ya vifaa vipya kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kampuni yake ya utengenezaji wa filamu  iliyopo pale TZ.

Kanumba akiwa ndani ya duka la B&H New york

Duka la B&H kwa nje

Cameras katika moja ya kitengo cha duka hilo

Kanumba akitoka na baadhi ya vitu alivyo nunua


Mbali na The Greatest kuwa likizo USA kazi zinaendelea kama kawaida ofisini kwake na mwezi huu kwa kuanza mwaka anaanza na movie iitwayo...''DECEPTION, movie hii ina tarajiwa kuwa mtaani soon...Kanumba ameongeza kwa kusema hivi". Kwa mashabiki wa kweli na wazalendo inatakiwa kununua copy original na si feki,lakini pia hawaazimani bali kila mtu hununua ya kwake tena original.''Mkataa kwao ni mtumwa''..''Mcheza kwao hutunzwa'' ''Tusitukuze vya nje na kudharau vyetu maana upendo wa dhati huanzia nyumbani na si ugenini,tujikubali sisi wenyewe kwa kupeana mioyo na kushauriana kwa njia na nia njema bila kutukanana wala kupondana maana lengo letu ni zuri kwa jamii aliongeza msanii huyo
PATA NAKALA YAKO MAPEMA
kwa habari zaidi unaweza kumtembelea kwenye link hizi; http://kanumbathegreat.blogspot.com/ na pia katika wesite yake hapa;  www.kanumba.com


Proposed changes to student rules, Post Study Work graduates & their dependants.-UK

The government announced consultation on proposals for changes on the student visa. The intention of the proposal was to build on recent changes to the points-based system to make it more transparent and flexible. The consultation has already started and is due to close on 31st January 2011. The findings and changes will be announced thereafter. The changes will affect students, those on Post Study Work and their dependants.

The proposed changes as follows.
Ø Minimum level of course & Type of sponsor
Currently only Highly trusted institutions are allowed to offer courses below NQF level 3. All other sponsors are allowed to offer courses from level 4 to degree level. Under the new proposals, all courses below level 6 (degree level) will only be offered by Highly Trusted Institution. However, all courses above level 6 can be offered by other institutions.

Ø English Language requirements
Since August 2010, all Tier 4 (General) students wishing to undertake a course of studybelow degree level (excluding English language students) have had to pass a secure English language test to demonstrate proficiency at level B1 on the Common European Framework of Reference for languages (CEFR), an intermediate level of language competency. They have to demonstrate competence at B1 level in reading, writing, speaking and listening. With the new proposals, all courses will require students to undertake the English test to minimum B2 level.

Ø Extension of leave in the UK
Currently students can extend their leave in the UK. However with the new proposal, Students will not be able t extend their leave in the UK. They must return home and apply for entry overseas when they finish their course and they must demonstrate intention to study at a higher level on return.

Ø Post Study work.
The post study work will be closed however students will be able to switch to tier 2 if they have job offer. Students on these programmes should start looking for jobs that fall under the Tier 2 and switch immediately as they may not be able to switch back to student visa when they new student rules are introduced. It’s important for students on PSW to consider switching early as the labour test rules do not apply. However to be able to switch they must have a certificate of sponsorship from a licensed sponsor.

Ø Permission to work
Currently students on degree levels and above are allowed to work 20 hrs term time and 40 hours during vacations. Those on courses below degree levels are allowed to work 10 hours term time. The new proposal will only allow student to work on campus during week days and during week ends they can work as many hours as they wish and also during the vacations they can work as many hours as they wish. Those on study to work will be on a 66:33 ratio.

Ø Dependants & working requirements
Currently dependants of students studying below NQF level 6 are limited to work whilst those above level 6 are allowed to work in the UK. Additionally only students studying for more than 12mnths courses are allowed to come to the UK. Under the proposals, Students will only be able to bring their dependant to UK if their courses are for are more than 12 months. However the dependants will no longer be allowed to work unless they can be able to switch to tier 1 or 2 in their own rights.

Ø Documentary evidence for Qualification and Maintenance requirement
Currently students have to prove that they have sufficient funds to maintain themselves without seeking recourse to public funds using their bank statements for a specific period of time. They are also required to provide their certificates to confirm their progress and/or previous qualifications. Under the proposed changes, Lower risk students can self-declare that they can meet the maintenance requirement & hold specified qualifications. However higher risk students must provide original documents as now to demonstrate maintenance & previous qualifications. To differentiate the two classes High & Low risk, it’s proposed that this should be according to sponsor rating.

NB:
The proposals are still on going and the closing date for the responses is 31st January 2011. The response and final decisions are intended to be announced as soon as possible thereafter these dates.
Its important that students and those on PSW take action and prepare for the new changes and the impact on their current status especially those studying courses below degree level in institutions that are rated below Highly trusted and/or those whose visas are about to expire but they have not finished their courses as they may be required to leave the UK and apply from outside the UK. Where this is the case, the students must note that from outside the UK entry clearance will only be given to courses above degree level.

The changes will also have an effect on those on PSW if they do not prepare to switch to Tier 2 as soon as possible before their leave expire as they may not be able to switch to Tier 4 at the end of their leave should the proposal for the new changes be approved and effected.

Also those with dependants in the UK should note the proposed changes to working requirements that dependants need qualify in their own rights under Tier 1 & 2 to be able to work in the UK.

source:
Director Of Communication.

CCM Branch -Reading ,Berkshire .United Kingdom
Telephone No:+447876126862

19 January 2011

WALID TANZANIAN RAPER WHO REPS TZEE 4 REAL NDANI YA HOLLAND



Thax to Nick Wakweli-Holland

HAPPY BIRTHDAY SEAN MACLEAN-SCOTLAND UK

SEAN MACLEAN having fun with other children 

Birthday boy" Sean Maclean" with his guiter,The future JIMMY HENDRIX!!.
Your Mum & Daddy , family an HUNGAZ we wishing you a good health and long life in the future.INSHALAH!!!!
(Salaaam toka kwa mama yako mzazi bi Sakina Maclean)


JUNYMAN BEHIND THE SCENE-VIDEO PART-1

SIMU MPYA YA NOKIA 2011 YATOKA KUKIDHI MAHITAJI YA WA SOUTH AFRICA


Simu hii imetengenezwa special kwa ajili ya kujikinga na waporaji ambao wamekithiri pale South Africa.Kazi kweli kweli.Mdau aliyetuma ujumbe huu amesema watu walipangana kwa foleni ilikujipatia simu hiii na hali ya uporaji kwa sasa inasemekana kupungua kwani usalama na mawasiliano yameongezeka.

18 January 2011

MAGAZETINI LEO 18/01/11

Na Kassano Mushumbusi Jonathan

NIPASHE…… Katiba Mpya, Dowans mtihani wa Makinda, Atazamwa aamue hoja binafsi za wabunge, Ni Dowans ya kafulila, Katiba ya Mnyika…..Hali yachafuka vyuo vikuu….KCMC yazidiwa, wagonjwa walia…..Polisi wahaha kuibwa dawa za kulevya kituoni…..Meya na mkakati wake wa kuingálisha Kinondoni…..
HABARI LEO…… Dawa ya mgawo wa umeme yaja, kampuni yaja kuzalisha nishati hiyo kwa makaa ya mawe, Ufuaji wa megawati 600 kuingia kwenye gridi karibuni….Pinda atoa maagizo kwa watendaji…..’Wanasiasi msiichafue Arusha”……Wawili wafa mgodini….Albino aliyekatwa miguu…..Man United yaikamia Chelsea…..

TANZANIAN DAIMA….. Slaa: Tutajibu mapigo, waandaa mkanda kamili wa video ya Arusha, Lengo ni kujibu ‘uchakachuaji wa Polisi”……Askari wa ujangili akutwa na pembe za faru wa JK……Mgomo wanukia Mkwawa, Kisa ni kuchelewa kwa fedha zao za mikopo…..Pinda apiga marufuku mifuko ya plastiki……

MWANANCHI…… Pembe za faru wa JK zabambwa MZA, Mmoja wa watuhumiwa ni ofisa wa wanyamapori……Spika akuna kichwa kuikabili Dowans……Khanga, viroba vyama madawati shuleni Dar…..Maofisa wa CAG kutinga UDOM leo…… Profesa safari angátuka CUF……Baba adaiwa kumuua mwanaye, kumzika…..

KUWA MTALII KTK NCHI YAKO KWA BEI POA


Waydaeli Josephat
 Hi,leo ninakuja hapa na swala 1 tu.Hivi mnajua kuwa nchi yetu ina vivutio vingi sana.Kama Mlima kilimanjaro,mbuga na wanyama na mengineyo ambayo yana2patiawatalii kutoka sehemu mbali mbali,ila jamani kwa nn na cc watz 2cwe watalii?kutokana na hilo Tanzanian group 2meandaa trip ya kwenda kuangalia mbuga ya wanyama ya Mikumi kwa sh 50,000 2 utaweza kwenda kutembeleambuga hizo.Karibuni sanaa.unaruhusiwa kuuliza maswali.

Trip hii itakuwa tarehe 26 na 27 mwezi 2/2011. kwa sh 50,000 utakuwa umelipia nauli ya kwenda na kurudi pamoja na sehemu ya kulala... kwa swala la chakula na vinywaji tumeona ni bora watu wajitegemee...tunategemea kukodi mabasi ya kutupeleka huko..
tiketi zimeanza kuuzwa na zina mwisho wake, ili tuweze kulipia mabasi mapema na kuwa na uhakika na kiasi cha watu watakaoenda...
karibuni sana na unaruhusiwa kumjulisha na mwingine.
kwa maelezo zaidi uliza nami ntakupatia..(.From..Tanzania group)

NB:Unaweza kumtumia ujumbe dada huyu kupitia mtandao huu pia email: hungazblog@gmail.com au toa maoni yako hapo chini kisha nitayawakilisha .

17 January 2011

SERIKALI YATANGAZA AJIRA 9,226 KWA WAALIMU WA SEKONDARI NA VYUO




Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kati) akitangaza ajira kwa waalimu
Katika mwaka wa masomo 2009/10 jumla ya wanafunzi 19,652 walihitimu mafunzo ya ualimu wakiwemo ngazi ya shahada 12,120 na stashahada 7,532. Kati ya wanafunzi hao jumla ya wanafunzi 17,684 walihitimu na kufaulu masomo yao, wenye shahada wakiwa 12,095 na wenye stashahada 5,589.

Uchambuzi wa sifa za wahitimu 17,684 waliohitimu na kufaulu mitihani yao umeonesha kuwa jumla ya wahitimu 8,857 wametoka kazini (in-service). Idadi hiyo inajumuisha wenye shahada 7,437 (25 kutoka Zanzibar) na wenye stashahada 1,420. Walimu hao wamerudi kwa waajiri wao ili wapangiwe kazi kulingana na elimu yao. Aidha, kuna wahitimu 328 kutoka Zanzibar (wakiwemo 303 tarajali na 25 kutoka kazini) ambao wanatarajiwa kuajiriwa katika shule na vyuo vya Zanzibar.Hivyo, wahitimu wanaobakia ambao wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu Tanzania Bara ni 8,524 wakiwemo wenye shahada 4,355 na wenye stashahada 4,169.

Kama ilivyobainishwa katika sehemu ya kwanza ya taarifa hii, jumla ya wahitimu 8,524 waliohitimu na kufaulu mitihani yao wataajiriwa na Serikali katika mwaka huu wa fedha. Vilevile Serikali imekubali kuajiri walimu 702 (wakiwemo 565 wenye shahada na 137 wenye stashahada) waliomaliza mafunzo yao miaka ya nyuma ambao wameomba kuajiriwa Serikalini.

Hivyo, jumla ya walimu wote watakaoajiriwa Serikalini kwa mwaka wa fedha 2010/2011 ni 9,226 wakiwemo wenye shahada 4,920 na wenye stashahada ni 4,306. Kati ya walimu watakaoajiriwa jumla ya walimu 9,039 wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na walimu 187 wamepangwa kufundisha katika vyuo vya ualimu.

Walimu wote wa shule za sekondari wamepangwa katika Halmashauri mbalimbali kwa kutumia kigezo cha upungufu wa walimu katika Halmashauri husika. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kuripoti katika Halmashauri aliyopangwa kwa kuwa fedha za mshahara wake zimekasimiwa kwenye Halmashauri alikopangwa na si vinginevyo.Orodha ya walimu hao na Halmashauri walikopangwa zimetumwa kwenye Mikoa na Halmashauri. Aidha, orodha hiyo inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (www.pmoralg.go.tz).
Walimu wote wapya wanaagizwa kuhakikisha kwamba wanaripoti katika Halmashauri/ Vyuo vya Ualimu walikopangwa ifikapo tarehe 24/01/2011. Watendaji na wasimamizi wa elimu kwenye Halmashauri na Vyuo vya Ualimu watakuwepo kuwapokea.

Mwalimu yeyote atakayeshindwa kuripoti kwenye Halmashauri / Chuo alikopangwa baada ya siku saba (7) tangu tarehe anayotakiwa kuripoti atahesabika kuwa amekataa kukubali nafasi ya ajira aliyopewa na Serikali.

Baada ya kuripoti kwenye Halmashauri/Vyuo waajiri watatakiwa kuwajazia walimu hao Fomu maalum zenye Taarifa ya Kiutumishi ya Mtumishi (Personal Data Form) na kuziwasilisha Ofisi ya Rais, UTUMISHI pamoja na barua ya ajira ya mtumishi. Taarifa hizo zikiwa katika “hard” na “soft copy” ziwasilishwe UTUMISHI kabla au ifikapo tarehe 29/01/2011 ili watumishi hao waingizwe katika mfumo wa malipo (Payroll). Waajiri wanakumbushwa kwamba “Computer Data Sheet” hazitahitajika katika zoezi hili.

Waajiri (Wakurugenzi wa Halmashauri na Katibu Mkuu – Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi) watawalipa malipo stahili kwa mujibu wa nyaraka na miongozo ya Serikali kuhusu waajiriwa wapya.

Nawatakia utumishi mwema katika Sekta ya Elimu.

Imetolewa na:
MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA
(WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI)

Imetufikia kupitia:
Director Of Communication
CCM Branch -Reading ,Berkshire .United Kingdom
Telephone No:+447876126862

BAADA YA KIMBEMBE CHA DC WAZIRI MKUU ATATUA MGOGORO WA UDOM

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na wanachuo wanaochukua fani ya utabibu katika Chuo Kikuu cha Dodoma alipotembelea chuoni hapo kusikiliza matatizo yanayowakabili na kuyapatia ufumbuzi
Baada ya mkuu wa wilaya ya Dodoma  kuwekwa chini ya ulinzi na wanafunzi wa chuo hicho,Waziri mkuu Mh Mizengo Pinda alitia timu jana na kuweka sawa utata uliokuwa unakikabili chuo hicho.Wahadhiri ambao waligoma kwa kutetea maslahi yao wanatarajia kuanza masomo leo.Kutokana na taarifa toka ktk ofisi ya waziri mkuu,Madai ya wahadhiri hao ambayo mojawapo ni kulipwa malipo ya posho zao, Yaliahidiwa kutekelezwa na ofisi hiyo punde mwezi Februari 2011.Mbali na hayo ofisi hiyo itamuagiza Mkaguzi mkuu wa mahesabu wa serikali(CAG) kuchunguza swala la jinsi mahera hayo yalivyo tumika chuoni hapo.

TAARIFA TOKA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA

Akizungumza na wanajumuiya ya wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) jana mchana kwenye ukumbi wa Chimwaga, Waziri Mkuu alisema matatizo yaliyojitokeza katika chuo hicho ni mlundikano wa mambo ambayo yamekuwepo siku nyingi lakini mengi ni ya kiutendaji tu na yanaweza kuisha bila kupoteza muda mwingi.

“Nimeongea na viongozi wa UDOMASA na kuwaahidi kuwa madai yenu ya posho yanaweza kukamilika mwezi Februari, nilitaka yaishe mwezi huu lakini kwa taratibu za HAZINA sasa hivi wameshaanza kushughulikia mishahara ya Januari kwa hiyo marekebisho yenu hayawezi kuwahi…wameniahidi mwezi ujao yatakamilika”, alisema huku akishangiliwa.

Amesema amemwita Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aje kukagua taarifa za mahesabu ya chuo hicho ili kubaini tuhuma zilizojitokeza za watu kulipwa hundi mbili za mishahara,walioacha kazi kuendelea kuwemo kwenye payroll ya mishahara, na wengine kukosekana kabisa kwenye payroll.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba CAG atakuwa hapa kesho… mpeni ushirikiano ili aifanye kazi kwa urahisi…, nia yetu ni kuangalia mfumo mzima wa fedha na utawala ukoje ili ikibidi uweze kurekebishwa,”alisema.

Kuhusu madai ya wanafunzi ya tatizo la maji, Waziri Mkuu alisema amemwagiza Naibu Katibu Mkuu (Fedha) Bw. John Haule ambaye alikuwepo katika ukumbi wa Chimwaga afuatilie uhamisho wa ndani wa fedha (reallocation) katika Wizara ya Maji ili zipatikane sh. bilioni 1.66 zinazohitajiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dodoma (DUWASA) kuchimba visima maeneo ya Ng’ong’ona na Ihumwa ikiwa ni pamoja na kutandaza mabomba hadi chuoni ili kupunguza shida ya maji haraka iwezekanavyo.

Pia alisema katika mipango ya muda mrefu, DUWASA pia wanataraji kupata dola za Marekani milioni 26 ambazo zitatumika kuchimba visima vingine na kujenga matanki yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 12 za maji na hivyo kuondoa kabisa tatizo la maji chuoni hapo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idris Kikula alimweleza Waziri Mkuu kwamba mahitaji halisi ya maji chuoni hapo ni lita milioni 3.5 kwa siku ambazo kati ya hizo, lita milioni 1.5 ni kwa matumizi ya wanafunzi peke yao na lita nyingine milioni mbili ni kwa matumizi ya ujenzi wa majengo unaoendelea chuoni hapo.

Mapema akizungumza na Kamati ya Makatibu Wakuu iliyoundwa na Katibu Mkuu Kiongozi, mara baada ya kuwasili mjini Dodoma jana asubuhi, Waziri Mkuu alielezwa kwamba kuna matatizo ya malipo ya posho na mishahara kwa watumishi na wahadhiri wa chuo hicho.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Bw. Idd Mwerange alimwahidi Waziri Mkuu kwamba watarudi madarasani wakati wakisubiri madai yao yakamilishwe bali aliomba kuwe na uwakilishi wa UDOMASA katika timu ya watu watakaonana na CAG.

Akifunga mkutano huo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idris Kikula alimwahidi Waziri Mkuu kwamba maagizo yake yatafuatiliwa na kwamba kesho (Jumatatu) menejimenti, idara ya Uhasibu na UDOMASA watakutana ili kuunda timu ya pamoja ambayo itakaa na kubainisha stahili za walimu wote ili orodha hiyo iwasilishwe kwa Waziri Mkuu mapema iwezekanavyo kwa ufuatiliaji.

Katika ziara yake ya jana, Mh. Waziri Mkuu alifanya vikao viwili, kimoja kikiwa cha uongozi wa Chuo Kikuu cha UDOM na kingine cha Serikali ya wanafunzi ambavyo vilidumu hadi saa 12.30 jioni na kumlazimu kuahirisha vikao viwili vilivyobaki hadi leo.

Kwa mujibu wa ratiba ya Chuo hicho,mara baada ya kukutana na serikali ya wanafunzi, Waziri Mkuu alipangiwa kukutana na jumuiya ya wanataaluma wa Chuo hicho (UDOMASA) na kisha kufanya majumuisho katika ukumbi wa Chimwaga kwa kuzihusisha pande zote tatu.

Katika vikao vyote viwili, Waziri Mkuu alielezwa matatizo yanayokibabili chuo hicho makubwa yakiwa ni uhaba wa maji, uhaba wa walimu, vifaa vya masomo na mlundikano katika mabweni.

Waziri Mkuu kabla ya kufanya mikutano hiyo miwili, alifanya ziara chuoni kukagua miundombinu ya maji safi, maji taka,vyumba vya kulala katika mabweni ya Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii pamoja na mabweni ya skuli ya Tiba na Uuguzi pamoja na ujenzi wa visima vya maji.

Chanzo:Global publishers

MKUU WA WILAYA AWEKWA CHINI YA ULINZI DODOMA UNIVERSITY

Chuo Kikuu cha Dodoma
MGOMO wa wanafunzi na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) umechukua sura mpya baada ya wanachuo hao kumteka na kumweka chini ya ulinzi kwa saa nne Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, John Tupa, wakitaka wamuone Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Tukio hili la aina yake lilitokea 15/01/11 mchana na kuvuruga hali ya usalama katika eneo hilo hivyo kumlazimisha Pinda ambaye alikuwa akifanya mazungumzo na menejimenti ya chuo hicho kuondoka kupitia njia nyingine akiwa chini ya ulinzi mkali.

Tupa aliingia katika mikono ya wanafunzi saa saba mchana katika eneo Chimwaga alipoenda chuoni hapo kufanya maandalizi ya kumpokea Waziri Mkuu Pinda ambaye wakati huo alikuwa kwenye kikao na uongozi wa chuo katika jengo la utawala lililopo umbali unaokadiriwa kuwa kilomita mbili.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, baada wanafunzi kulizingira gari la DC Tupa walitoa upepo kwenye matairi yote ya gari lake huku wakipaza sauti kuwa hawatamwachia mpaka Waziri Mkuu Pinda afike katika eneo hilo.
Kundi hilo la wanafunzi ambalo lilikuwa likitoa vitisho kwa Tupa lilimfanya dereva wake ambaye alifanikiwa kutoka kwenye gari kukimbia na kumuacha bosi wake akiwa chini ya ulinzi wa wanachuo hao.
Awali, Pinda alipowasili chuoni hapo alipokelewa kwa shangwe na umati mkubwa wa wanafunzi wakiwa pamoja na wahadhiri.
.....endelea hapa
Chanzo:Mtandao wa mwanachi

16 January 2011

JUNYMAN VIDEO SHOOTING TOKA KUNDI LA M2S ILIKUWA HIVI

Jana 15/01/2011 mishale ya saa 6 na nusu za mchana Mitaa ya Barking London Msanii wa kizazi kipya mwenye maskani yake hapa UK london aligonga video yake ya kwanza ya Nyimbo yake iitwayo JUNY!!!!.Video hii ambayo nia utambulisho wa msanii huyu mahiri ni moja katika harakati ya kuandaa Ujio wa album yake ambayo itatoka hivi karibuni.JUNYMAN ni mmoja wa wasanii wanaounda kundi kubwa la MONSTERZ linalo julikana kwa jina la """M2S""
Hungaz nilidokezwa na msanii huyu kuwa video hiyo inaweza kukamilika ndani ya wiki moja.chini ya kampuni ya MUSSA PRODUCTIONS ya Ealing Broadway West London.

Monsters,Junyman(orange overoll) wakipozi tayari kwa kazi

Chemicali (left) na Junyman(Monster face masked)


Mussa Productions na Junyman

Chemicali na Junyman

Mussa Productions wakikamua

Full kujiachia


Picha zikiendelea

Chemicali na Junyman nxt catch

Monsterz

Stay tuned for BEHIND THE SCENE coming soooon!!!
Picha kwa hisani ya Junyman na M2S

14 January 2011

HABARI-TBC 14/01/11 ELIMU YA MSINGI KWA WATOTO WA KIMASAI YAVUTIA WATALII



JE MTAZAMAJI UMEJIFUNZA NINI? NA JE KWELI SERIKALI INASHIDWA KUWAJENGEA WATOTO HAWA DARASA LA KIUKWELI JAMANI???

SPECIAL OFFER FROM VINCENT RESTAURANT-READING

EVERY MONDAY-THURSDAY
 SPEND £5 @ THE BAR & GET FREE SOUP
EVERY FRIDAY-SUNDAY
SPEND £5 @THE BAR & GET FREE NYAMA CHOMA

MUSIC TILL LATE
NYAMA CHOMA SERVED EVERYDAY OF THE WEEK
YOUR ALL WELCOME
For more details  contact :(Gardol 07796923838)

13 January 2011

Unbeatable Price to Dar Es Salaaam


Locus Impex Shipping
WE SHIP ALL TYPES OF CARGO TO AFRICA AT UNBEATABLE RATES, i.e CONTAINERS, TRUCKS, CARS, MACHINES,TRACTORS ETC.WE ALSO SELL USED VEHICLES & MACHINERY FROM UK.

40' CONTAINER TO DAR from £2,200
20' CONTAINER TO DAR from £1,300

Our sale ends on 31/01/2011 Midnight. For more information do not hesitate to contact us.

Bernard Chisumo
Marketing Director ,Reading Branch
Locus International Ltd
14 Rothwell Walk,Caversham Reading,RG4 5DB
Tel: +44 118 954 5890 or 07876126862
Email: bchisumo74@yahoo.com, reading@locusimpex.com

www.locusimpex.com

VIDEO SHOOTING YA MSANII ANAYEIBUKIA KUTWANGWA SIKU YA JOMAMOSI 15/01

SAFI(the queen),JUNYMAN na CHEMICALI

KUTAKUWA KUNA VIDEO SHOOTIN YA {JUNY MAN}
SIKU YA JUMAMOSI 15/01/2011...@..BARKING..LONDON
KUANZIA SAA NNE {10am} ASUBUHI MPAKA JUWA KUZAMA...
DRESS CODE NI T-SHIRT NYEUPE AU NYEUSI...
NYOTE MNAKARIBISHWA. KWA ATAKAYEPENDA KUSHIRIKI WASILIANA NA  HUNGAZ  (07551447855) , JUNYMAN on(07947754854)................M2S

SHEREHE ZA MIAKA 47 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kushoto) wakiwa wamesimama kupokea maandamano ya wawakilishi wa wananchi kutoka mikoa mbalimbali za Zanzibar kwa ajili ya kusherekea ya miaka 47 ya Mapinduzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima kuadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan huko Unguja jana.
Kwa taarifa kamili soma hapa: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/sherehe-za-miaka-47-ya

12 January 2011

THE ONLY PLACE TO GO ON YOUR VALENTINES DAY IS!!!!!!!!


where will u be? Sat 19thFeb Valentines weekend..its going down in Reading town..@the only place 2 be PLUG n PLAY rg1 8lg U KNOW HOW WE GET DOWN!!!!RichieDee,John plus guest djs will be on the 1 and 2!Straight Flavas for ally'all.Get involved its official


MR BILINGUAL'S MESSAGE TO HIS FANS ABOUT HIS FLOWCTUATION MIXTAPE



Mr Bilingual
I know I know, I'm late!!.

Sorry guys, I've been MIA for a while. Life is so busy, I'm having a hard time keeping track of my days
But here we are again, it's a NEW YEAR, so we need to make NEW and BETTER moves.
My new Tape Flowctuation will be available soon, and this time it's for real, so stay tuned!!
And I am planning on putting out a lot more music in the near future, so you will all here from me!! Again, HAPPY NEW YEAR and GOD bless you ALL!!! ---F.A.
Visit his website on  www.mrbilingual.com  and get to know him.
You can join him on facebook following this link http://www.facebook.com/mrbilingual.
Hey Bilingual,! hungaz we thank you for been in touch.Keep it up man and lets keep it real.Big up to all ya crew and fame,Dont forget ma Hommie STANBOI The African Child.We cant wait to hear from u Bro again!!!Bless

50 cent signs Gamu????

GAMU NHENGU aka Miss Gamuchirai


50 Cent has reportedly signed ‘X Factor' reject Gamu Nhengu to his new record label.

Her deal is said to be with the newly launched G-Note Records, under the name Miss Gamuchirai.
"Miss Gamuchirai has been singed to 50 Cent's new record label, G-Note," said a source.
"G-Note will focus on 50's favourite acts that don't fit neatly into G-Unit's hip-hop categorisation and will favour pop and R&B artists."
It's also thought that Fiddy had to wrangle with her ‘X Factor' contract before getting her signature.
"It is believed that many labels have been interested in signing Gamu but G-Note offered the best deal and are best connected to make her dreams reality," they added.
Gamu was sensationally passed over by Cheryl Cole at the Judge's Houses stage of 'The X Factor' in favour of Cher Lloyd and Katie Waissel.
It later emerged that Gamu faced deportation back to her native Zimbabwe after her family's visa reportedly expired. [MTV]--By Bern Anorld

11 January 2011

Pinda amkomalia Mwema sakata la Arusha


MH PINDA
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameingilia kati vurugu zilizotokea Arusha kutokana na mvutano wa kisiasa baina ya CCM na Chadema kuhusu suala la Meya wa Jiji la Arusha akitaka kuwapo suluhisho la kudumu baina ya pande mbili hizo. .....soma zaidi hapa

MEMORIAL OF SOPHIA GELARD LUSINGU

A memory is like a snapshop pictures, it captures every laughters and every teardrops, just so you know; it is never been missed out.


Sophia Lusingu
IT IS ONE YEAR EXACTLY TODAY SINCE OUR DEAR WIFE, MOTHER, SISTER FRIEND AND RELATIVE MRS. SOPHIA GERALD LUSINGU DEPARTED FROM OUR COMPANY ON 10 JANUARY 2009 AT 12:35PM AND YET THE PAIN AND MEMORY SEEMS LIKE YESTERDAY.

SOMEWHERE BENEATH THE SUNSET, WHERE LOVELINESS NEVER DIES, YOU DWELL IN A BEAUTIFUL GARDEN BENEATH THE BLUE OF THE SKY, AND WE WHO LOVE YOU AND MISS YOU, WHOSE PARTING CAUSED GREAT PAIN, WILL LIVE IN OUR HEARTS FOREVER UNTIL WE MEET AGAIN.

DEARLY LOVED, SADLY MISSED BY YOUR HUSBAND GERALD, YOUR DAUGHTER SAMI, FAMILY AND FRIENDS.

7 January 2011

HAPPY BIRTHDAY SHEIN RANGERS FOOTBALL CLUB 'S BLOG


Bonyeza hapa : http://sheinrangers.blogspot.com/
 Leo siku ya tarehe 7 January 2011 Blog hii inatimiaza miaka miwili toka kuanzishwa kwake.

Uongozi wa timu ya Shein Rangers Sports Club unapenda kutoa shukurani kwa wadau mbali mbali wanaotembelea blog hii na kutoa maoni yao, wapenzi wa michezo, blog mbali mbali marafiki na viongozi wa vilabu vya michezo marafiki na wadau wakubwa wa blog hii.
Kwa kipindi cha miaka miwili idadi ya wasomaji wa blog hii imeongezeka mara tatu zaidi ya mwaka jana na pia kwa sasa blog hii ina link na mitandao mbali mbali duniani ikiwemo mtandao maarufu duniani wa facebook.
Hapa chini tumeandaa picha na matukio muhimu yaliyoripotiwa na blog hii kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Mwaka 2010 timu ya Shein Rangers iliweza kutwaa ubingwa wa UKIMWI DAY CUP 2010 mashindano yaliyoshirikisha timu na vituo mbali mbali vya michezo vya mkoa wa Dar es salaam.
Click here see more pictrure

6 January 2011

DAMU YA MWAGIKA KWENYE MAANDAMANO YA KATIBA TANZANIA(VIDEO-TBC)



NANI ALAUMIWE???

WAWILI WAUWAWA:
Jamani kwani lazima watu wafe kwa ajili ya haki zao? sasa serikali iko madarakani kwa ajili ya kulinda na kuwatumikia raia au kuwaua?? eti TANZANIA ni  nchi ya amani? kweli?..pata full habari tika kwa kamanda wa Arusha Bw Thobias Andengenye ,

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha
Thobias Andengenye


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye amethibitisha kuwa watu wawili wamekufa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia mapambano kati ya polisi na watu waliokuwa wanashiriki maandamano yasiyo na kibali ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA mjini Arusha siku ya Jumatano

Hata hivyo mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Arusha, Salash Toure akizungumza na TBC amesema amepokea miili mitatu mmoja ukiwa na majeraha ya risasi na majeruhi ishirini na tisa. Tayari miili miwili imetambuliwa.
Kamanda Andengenye amesema watu kumi na mmoja wanashikiliwa na polisi ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Wilbroad Slaa, mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na kwamba watuhumiwa wanafikishwa mahakamani hii leo mjini Arusha.
Katika maandamano hayo yaliongozwa na viongozi waandamizi wa CHADEMA polisi ililazimika kupiga mabomu na kuziba baadhi ya barabara za mji wa Arusha kwa zaidi ya saa mbili ikiwemo ile inayoelekea kituo kikuu cha polisi kufuatia baadhi ya waandamanaji kuvamia eneo hilo na kuanza kurusha mawe.
Mwandishi wa TBC Secelela Kongola aliyekuwa anafutialia tafrani ya maandamano hayo amesema purukushani za maandamano hayo zilizuruga shughuli za kawaida katika mji huo wa Arusha ambao ni maarufu kwa shughuli za utalii.

Chanzo: Sechelela Kongola, Arusha

TANZANIA GROUP NDANI UMMRA MAGOMENI MWEMBECHAI SIKU YA 1/1/2011 NA YATIMA

Nembo ya kikundi cha vijana wa Kitanzania kupitia muungano wao kwenye facebook
 (FACEBOOK TANZANIAN GROUP)

Katika kile kinachoonyesha kuwa Vijana nchini wanazidi kupata mwamko juu ya matatizo yenye kuwapata vijana wenzao katika sehemu mbalimbali, Wadau wa Tanzanian Group, ambao ni mjumuiko wa marafiki wenye kuunganishwa na mtandao jamii wa Facebook, waliungana na watoto waishio katika mazingira magumu wanaotunzwa katika kituo cha watoto yatima cha Ummra kilichoko Magomeni Mikumi, kusherehekea mwaka mpya pamoja nao.




Kassano Mushumbusi Jonathan, mmoja wa wasimamizi/waratibu wa kikundi hicho waliliambia Jukwaa Huru kwamba, pamoja na msaada kidogo walio peleka kituoni hapo, ikiwa ni michango toka kwa wadau walio ndani na nje ya kundi hilo, lengo lao jingine ni kujaribu kuwa karibu na vijana waishio kituoni hapo ili kuwaonyesha upendo ambao wanahisi wameukosa kwenye jamii na hivyo kujiona kama wao wana makosa.


“Tumepeleka msaada kidogo, kulingana na mwitikio wa wadau walio ndani na nje ya kundi hilo, lakini pia dhamira yetu kuu ni kwenda kukaa na vijana wale ambao kimsingi sisi tunaamini kuwa msada mkubwa wanaouhitaji ni mapenzi toka kwa vijana wenzao, na tunaamini kuwa kwa muda tutakaokaa nao tutawapa faraja kubwa kuwa wapo watu wenye kuwapenda huku mitaani licha ya kuwa hawana cha kuwasaidia kwa maana ya mali” amesema mratibu huyo.


Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na kile kinachoweza kuchukuliwa kama mwelekeo chanya wa mitandao jamii mbalimbali hapa nchini, ambapo imekuwa ikikusanya vijana ambao wamekuwa wakichagua kutumia umoja wao kwa malengo ya kimaendeleo zaidi tofauti na awali ambapo wengi walikuwa wakiitumia kwa mwelekeo hasi.


Bilashaka, umefikia wakati sasa wa Watanzania zaidi na hususan vijana ambao ndio watumiaji wakuu wa mitandao hii, kuhakikisha kuwa wanatumia fursa za namna hii kwa lengo la kuunda mitandao itakayokuja kuwaletea manufaa baadae, na kwa ziara kama hizi ni moja ya mambo ambayo jamii ikiyaunga mkono basi itawapa vijana msukumo wa kutumia mitandao hii kwa manufaa ya jamii zaidi kuliko kupotezana kimila na kiutamaduni.


Zawadi mbalimbali

misaada ya chakula na vinywaji n.k

Watoto wa UMMRA wakifurahia na Tanzania Group

Dada Waydaeli Josephat(TZ Group)akiwa na mmoja wa watoto

Watoto wakiburudika kwa kucheza muziki

Wana Tanzania Group ndani ya UMMRA 
Maana: "Mimi nimechangia kwa maskini na kukaribisha nawe pia-Tanzania Group"
Unaweza kuwatembelea vijana hawa katika ukurasa wao kwa kubonyeza hapa , na kuwasiliana nao zaidi ili kujua namna ya kuwasaidia au kushirikiana nao.
 Chanzo; Waydaeli Josephat(Tanzania Group)/Jukwaa kuu